Swali 32: Soksi za ngozi zinapanguswa namna gani?

Jibu: Namna ya kupangusa ni apitishe mikono yake kuanzia kwenye ncha ya vidole vya miguuni mpaka kwenye muundi wake. Kinachofutwa ni ile sehemu ya juu ya soksi za ngozi ndipo atapopitisha mikono yake kuanzia kwenye vidole vya miguuni mpaka kwenye muundi tu. Kupangusa kuwe kwa mikono miwili yote juu ya miguu yote; mkono wa kuume upanguse mguu wa kuume na mkono wa kushoto upanguse mguu wa kushoto kwa wakati mmoja kama inavofanywa wakati wa kupangusa masikio. Udhahiri wa Sunnah unaonyesha hivo. al-Mughiyrah bin Shu´bah (Radhiya Allaahu ´anh) amesema kuhusu kitendo cha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“… akapangusa juu yake [miguu miwili].”

Hakusema kuwa alianza kwa upande wa kuume. Alisema:

“… akapangusa juu yake [miguu miwili].”

Huu ndio udhahiri wa Sunnah.

Ikiwa tutakadiria mkono wake mmoja haufanyi kazki, basi hapo ataanza kwa upande wa kuume kabla ya wa kushoto. Watu wengi wanafuta mguu wa kuume kwa kutumia mikono yote miwili na mguu wa kushoto kwa kutumia mikono yote miwili. Kitu hiki hakina msingi kutokana na vile ninavojua. Wanazuoni wanasema kuwa apanguse mguu wa kuume kwa kutumia mkono wa kulia na apanguse mguu wa kushoto kwa kutumia mkono wa kushoto. Pasi na kuzingatia atafuta kwa njia gani itasihi. Lakini ninachozungumzia mimi ni ule ubora peke yake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Buhuuth wa Fataawaa fiyl-Mas´h ´alaal-Khuffayn, katika Majmuu´-ul-Fataawaa (11/177)
  • Imechapishwa: 06/05/2021