34. Mtu akiingiza mkono wake chini ya soksi unachenguka ule ufutaji wake?

Swali 34: Mtu akiingiza mkono wake chini ya soksi unachenguka ule ufutaji wake? Je, ufutaji unachenguka akizivua?

Jibu: Akiingiza mkono wake chini ya soksi ni sawa na hapana vibaya. Ule upangusaji hauchenguki kwa sababu hakuzivua.

Lakini akizivua, kutaangaliwa kama amevua au amefunua kiasi gani. Kama amevua au kufunua kiasi kidogo hakuna tatizo lolote.  Na kama amevua au kufunua sehemu kubwa kwa kiasi cha kwamba ikaonekana sehemu kubwa ya mguu, basi ule upangusaji wa huko mbele unabatilika.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Buhuuth wa Fataawaa fiyl-Mas´h ´alaal-Khuffayn, katika Majmuu´-ul-Fataawaa (11/178)
  • Imechapishwa: 06/05/2021