33. Mila ya Ibraahiym ni kumwabudu Allaah pekee na kujiepusha na shirki

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

nako ni kule kumuabudu Allaah pekee hali ya kumtakasia Yeye dini. 

MAELEZO

Nako ni kumwabudu Allaah pekee… – Hii ndio mila ya Ibraahiym: Kumwabudu Allaah pekee hali ya kumtakasia Yeye dini. Kwa msemo mwingine unatakiwa kukusanya kati ya mambo mawili: ´Ibaadah na Ikhlaasw. Yule mwenye kumwabudu Allaah na asimtakasie Yeye nia ´ibaadah yake itakuwa si chochote si lolote. Kwa msemo mwingine yule mwenye kumwabudu Allaah hali ya kufunga, kuhiji, kuswali, kufanya ´umrah, kutoa swadaqah, kutoa zakaah na akafanya matendo mengine. Lakini hata hivyo asimtakasie nia Allaah katika mambo hayo ima kwa sababu  ameyafanya yote hayo kwa kutaka kuonekana au kwa kutaka kusikika au kwa sababu amechanganya kitendo chake kwa kitu katika shirki kama mfano wa kumwomba asiyekuwa Allaah, kumtaka msaada asiyekuwa Allaah na kuchinja kwa ajili ya mwengine asiyekuwa Allaah, mtu huyu hakuwa ni mwenye kumtakasia nia Allaah katika ´ibaadah yake. Bali ni mshirikina na hayuko katika mila ya Ibraahiym (´alayhis-Salaam).

Watu wengi ambao wanajinasibisha na Uislamu hii leo wanatumbukia ndani ya shirki kubwa katika kumuomba asiyekuwa Allaah, kuyaabudu makaburi, kuyachinjia, kuyawekea nadhiri, kuyafanyia Twawaaf, kutafuta baraka kwayo, kuwaomba msaada wafu na mengineyo. Sambamba na hilo wanasema kuwa ni waislamu. Watu hawa hawakuijua mila ya Ibraahiym  (´alayhis-Salaam) ambayo ndio ambayo Mtume wao Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) yuko juu yake. Hawakuijua. Kuna uwezekano vilevile wameijua lakini wakaenda kinyume nayo kwa ujuzi, jambo ambalo ndio baya zaidi.

Mila ya Ibraahiym haikubali shirki kwa njia yoyote ile. Ambaye atachanganya kitendo chake na shirki hayuko katika mila ya Ibraahiym ijapokuwa atajinasibisha nayo na akadai kuwa ni muislamu. Lililo la lazima ni wewe kuitambua mila ya Ibraahiym, uitendee kazi, ushikamane nayo barabara kwa kumwabudu Allaah hali ya kumtakasia Yeye dini. Katika ´ibaadah yako kusiwe kitu katika shirki ndogo au shirki kubwa. Hii ndio mila ya Ibraahiym (´alayhis-Salaam) ambayo ni Haniyfiyyah iliyojiepusha na shirki kwa ukamilifu wake na ikaelekea Tawhiyd kwa ukamilifu wake. Inahusiana na kumwabudu Allaah pekee hali ya kumtakasia Yeye dini.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 73-74
  • Imechapishwa: 09/12/2020