33. Maumbo ya kichwa na ya mabega ya mwanamke hayatakiwi kuonekana

Kutokana na Aayah hizo mbili inabainika ya kwamba ni lazima kwa mwanamke wakati anapotoka nyumbani kwake kuvaa shungi na jilbaab juu ya mtandio. Kwa sababu, kama tulivyotangulia kusema, kufanya hivo kunamsitiri zaidi na uwezekano ni mdogo wa kuonekana maumbo ya kichwa na mabega yake, jambo ambalo linatakikana pia na Shari´ah. Namna hiyo ndivo ambavo baadhi ya Salaf wamefasiri Aayah ya kujiteremshia jilbaab. as-Suyuutwiy amesema:

”Ibn Abiy Haatim amepokea kutoka kwa Sa´iyd bin Jubayr alipokuwa akifasiri Aayah:

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ قُل لِّأَزْوَاجِكَ وَبَنَاتِكَ وَنِسَاء الْمُؤْمِنِينَ يُدْنِينَ عَلَيْهِنَّ مِن جَلَابِيبِهِنَّ

“Ee Nabii! Waambie wake zako na mabinti zako – na wanawake wa waumini – wajiteremshie Jilbaab zao.”

”Wajifunike kwa jilbaab zao ambazo zinawekwa juu ya shungi. Haifai kwa mwanamke wa Kiislamu kuonekana na mwanamke wa kando naye isipokuwa kama atakuwa na jilbaab juu ya shungi ambayo inafunika kichwa na kifua chake.”[1]

Kwa masikitiko makubwa ni kwamba wanawake wengi hii leo wana kasoro ya kuchanganya kati ya jilbaab na shungi; ima wakatoka nje na hali ya kuvaa jilbaab peke yake juu ya vichwa vyao au mtandio peke yake. Isitoshe daima haiwi ndefu ya kutosha. Shali za leo ni mfano wa nguo hizo kwa njia ya kwamba wakati mwingine nywele za paji la uso au shingo linakuwa wazi.

[1] ad-Durr al-Manthuur (5/222).

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 85
  • Imechapishwa: 18/09/2023