32. Namna ya kutangamana na mtu anayetaka kukata roho

Kinachotakikana kwa yule ambaye ana dhana yenye nguvu juu ya kwamba mgonjwa anataka kukata roho anatakiwa kumtunza kwa njia iliokuwa bora kabisa kutokana na mambo yatayomnufaisha katika kaburi lake na siku ya Qiyaamah. Akumbushe juu ya Aakhirah, amuamrishe kuacha wasia na kutubia na kumtamkisha shahaadah iwe ndio maneno yake ya mwisho. Kabla ya hayo anatakiwa kumkataza kujipiga kwenye mashavu, kuchana nguo, kujikokota nywele, kuomboleza na maneno na matendo mengine yaloharamishwa. Katika hali hii matarajio yake yanatakiwa kuwa ni yenye nguvu kuliko khofu yake na anatakiwa kuhakikisha ni mwenye kumhimidi sana Allaah na kusema “Hakika sisi ni wa Allaah na hakika sisi Kwake ni wenye kurejea” na kuwa radhi na Allaah (´Azza wa Jall).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Muhammad al-Hanbaliy al-Manbajiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasliyatu Ahl-il-Maswaa-ib, uk. 54
  • Imechapishwa: 14/10/2016