Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Mtu wa batili hawezi kuja na hoja yoyote isipokuwa katika Qur-aan kuna [dalili] inayoivunja na kubainisha ubatili wake. Kama alivyosema Allaah (Ta´ala):

وَلَا يَأْتُونَكَ بِمَثَلٍ إِلَّا جِئْنَاكَ بِالْحَقِّ وَأَحْسَنَ تَفْسِيرًا

“Na wala hawakujii kwa mfano wowote isipokuwa Tunakuletea haki na tafsiri nzuri kabisa.” (25:33)

Wamesema baadhi ya wafasiri, Aayah hii inajumuisha kila hoja ambayo watakuja nayo watu wa batili mpaka siku ya Qiyaamah.

MAELEZO

Mtu wa batili hawezi kuja na hoja juu ya batili yake, isipokuwa katika Qur-aan kuna chenye kufichukua hoja hii batilifu. Bali kila mtu wa batili anayekuja na hoja juu ya batili yake kutoka katika Qur-aan na Sunnah, dalili hii inakuwa dhidi yake. Haya yamesemwa na Shaykh-ul-Islaam (Rahimahu Allaah) katika utangulizi wa kitabu chake “Daar´ Ta´aarudhw-in-Naql wal-´Aql”.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 54
  • Imechapishwa: 04/11/2023