33. Mpwekeshaji atakuwa na hoja ya wazi na bainifu zaidi kuliko ya mshirikina

Mtunzi (Rahimahu Allaah) anathibitisha kuwa mtu mpwekeshaji atakuwa na hoja ya wazi na bainifu zaidi kuliko ya mshirikina, pasi na kujali ni ufaswaha na usomi kiasi gani atakuwa nao. Amesema (Ta´ala):

وَلَا يَأْتُونَكَ بِمَثَلٍ إِلَّا جِئْنَاكَ بِالْحَقِّ وَأَحْسَنَ تَفْسِيرًا

“Na wala hawakujii kwa mfano wowote isipokuwa Tunakuletea haki na tafsiri nzuri kabisa.” (25:33)

Hawatakujia kwa hoja yoyote dhidi yako ambayo wameivisha haki batili, isipokuwa Tunakuletea haki na tafsiri nzuri kabisa. Ndio maana mara nyingi utapata namna ambavyo Allaah (Ta´ala) anajibu maswali ya washirikina na ya wengine ili kuwabainishia watu haki. Kwa njia hiyo haki inakuwa bainifu kwa kila mtu.

Hata hivyo kuna jambo ambalo mtu anatakiwa kuwa makini nalo. Mtu hatakiwi kuingia katika mjadala wowote isipokuwa baada ya kujua hoja za huyo mwengine na amejiandaa vizuri ili kuzivunja na kuziraddi. Akijiingiza bila ya maandalizi haya, matokeo yake yatakuja kuwa mabaya. Isipokuwa kama Allaah anataka kinyume chake. Kama ambavyo mtu haingii katika uwanja wa vita dhidi ya maadui pasi na silaha na ujasiri.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 54-55
  • Imechapishwa: 04/11/2023