Shayk-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

”Sita ni kwamba Maswahabah (Radhiya Allaahu ‘anhum) waliwafasiria Qur-aan wale waliokuja baada yao. Mujaahid amesema:

”Nilisoma Qur-aan yote kwa Ibn ´Abbaas mara tatu; nikasimama kwenye kila Aayah na kumuuliza nayo.”[1]

Kwa ajili hiyo Sufyaan ath-Thawriy akasema:

”Ukipata tafsiri kutoka kwa Mujaahid, basi tosheka nayo.”[2]

Ibn Mas´uud alikuwa akisema:

“Kama ningelijua kuwa kuna mtu ambaye ana elimu zaidi wa Kitabu cha Allaah kuliko mimi, ningelimpanda ngamia kumwendea.”[3]

Kila mmoja katika wanafunzi wa Ibn Mas´uud na Ibn ´Abbaas kumanukuliwa kutoka kwao kiasi cha tafsiri ya kutosha. Isitoshe nukuu za Maswahabah na wanafunzi wao zimethibiti na zinatambulika juu ya jambo hilo kwa wanazuoni.”[4]

[1] Jaamiy´-ul-Bayaan (1/65) na Hilyat-ul-Awliyaa’ (3/279-280).

[2] Jaamiy´-ul-Bayaan (1/65).

[3] al-Bukhaariy (5002) na Muslim (2463).

[4] Majmuu´-ul-Fataawaa (5/157-159).

  • Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Allaamah ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad al-Badr
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Athar al-Mash-huur ´an-il-Imaam Maalik fiy Swifat-il-Istiwaa’, uk. 53-54
  • Imechapishwa: 02/12/2025