Shayk-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:
”Tatu amesema (Ta´ala):
إِنَّا أَنزَلْنَاهُ قُرْآنًا عَرَبِيًّا لَّعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ
”Hakika Sisi tumekiteremsha kikisomeka kwa kiarabu ili mpate kufahamu.”[1]
إِنَّا جَعَلْنَاهُ قُرْآنًا عَرَبِيًّا لَّعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ
”Hakika Sisi Tumeifanya Qur-aan kwa kiarabu ili mpate kutia akilini.”[2]
Akabainisha kuwa ameiteremsha kwa kiarabu ili ipate kufahamika, jambo ambalo halipatikani isipokuwa kwa kuelewa maana yake.
Nne ni kwamba amemsema vibaya yule ambaye haitii akili na akasema:
وَإِذَا قَرَأْتَ الْقُرْآنَ جَعَلْنَا بَيْنَكَ وَبَيْنَ الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِالْآخِرَةِ حِجَابًا مَّسْتُورًا وَجَعَلْنَا عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ أَكِنَّةً أَن يَفْقَهُوهُ وَفِي آذَانِهِمْ وَقْرًا
”Unaposoma Qur-aan Tunajaalia baina yako na baina ya wale wasioamini Aakhirah kizuizi kinachofunika, na tumetia juu ya nyoyo zao vifuniko waisweze kuifahamu.”[3]
فَمَالِ هَـٰؤُلَاءِ الْقَوْمِ لَا يَكَادُونَ يَفْقَهُونَ حَدِيثًا
“Basi wana nini hawa watu hawakaribi kufahamu yenye kuendelea?”[4]
Ingelikuwa waumini pia hawaitii akili, basi wangelikuwa ni wenye kushirikiana na makafiri na wanafiki katika yale ambayo Allaah amewasimanga kwayo.
Tano ni kwamba amewasimanga wale ambao wanaisikiliza tu bila ya kuifahamu na kuifanyia kazi. Amesema (Ta´ala):
وَمَثَلُ الَّذِينَ كَفَرُوا كَمَثَلِ الَّذِي يَنْعِقُ بِمَا لَا يَسْمَعُ إِلَّا دُعَاءً وَنِدَاءً ۚ صُمٌّ بُكْمٌ عُمْيٌ فَهُمْ لَا يَعْقِلُونَ
“Na mfano wa wale waliokufuru ni kama mfano wa yule ambaye anapiga kelele kwa asiyesikia ila wito na kelele tu [za wanyama anaowachunga]; viziwi, mabubu, vipofu kwa hiyo hawaelewi!”[5]
أَمْ تَحْسَبُ أَنَّ أَكْثَرَهُمْ يَسْمَعُونَ أَوْ يَعْقِلُونَ ۚ إِنْ هُمْ إِلَّا كَالْأَنْعَامِ ۖ بَلْ هُمْ أَضَلُّ سَبِيلًا
“Je, unadhania kwamba wengi wao wanasikia au wanatia akilini? Si vyenginevyo isipokuwa ni kama wanyama, bali wao wamepotea zaidi njia!”[6]
وَمِنْهُم مَّن يَسْتَمِعُ إِلَيْكَ حَتَّىٰ إِذَا خَرَجُوا مِنْ عِندِكَ قَالُوا لِلَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ مَاذَا قَالَ آنِفًا ۚ أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ طَبَعَ اللَّـهُ عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ وَاتَّبَعُوا أَهْوَاءَهُمْ
”Wapo miongoni mwao ambao wanakusikiliza kwa makini, mpaka wanapotoka kwako huwaambia wale waliopewa elimu: ”Amesema nini hivi punde?” Hao ndio ambao Allaah amewapiga muhuri juu ya nyoyo zao na wakafuata matamanio yao.”[7]
Wanafiki hawa wamesikia sauti ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) pasi na kumfahamu na kuhoji nini alichosema punde tu. Hivo ndivo anavosema yule ambaye hakufahamu maneno yake. Hivyo akasema (Ta´ala):
أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ طَبَعَ اللَّـهُ عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ وَاتَّبَعُوا أَهْوَاءَهُمْ
”Hao ndio ambao Allaah amewapiga muhuri juu ya nyoyo zao na wakafuata matamanio yao.”
Kwa hivyo yule mwenye kudai kwamba wale watu wa awali waliotangulia, ambao ni Wahajiri na Wanusuraji, na wale waliowafuata kwa wema kwamba hawafahamu maana ya Qur-aan, amewafanya ni sawa na makafiri na wanafiki katika yale ambayo Allaah (Ta´ala) amewasimanga kwayo.”[8]
[1] 12:02
[2] 43:3
[3] 17:45-46
[4] 4:78
[5] 2:171
[6] 25:44
[7] 47:16
[8] Majmuu´-ul-Fataawaa (5/157-159).
- Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Allaamah ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad al-Badr
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Athar al-Mash-huur ´an-il-Imaam Maalik fiy Swifat-il-Istiwaa’, uk. 52-53
- Imechapishwa: 02/12/2025

Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Allaamah ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad al-Badr
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Athar al-Mash-huur ´an-il-Imaam Maalik fiy Swifat-il-Istiwaa’, uk. 52-53
Imechapishwa: 02/12/2025
https://firqatunnajia.com/31-mwenye-kusimangwa-ni-yule-asiyeifahamu-qur-aan/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket