Miongoni mwa adabu za swawm ni kuharakisha kufungua pindi tu inapothibiti kuzama kwa jua. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Watu wataendelea kuwa katika kheri maadamu wanaharakisha kufungua.”[1]

Kuna maafikiano juu yake.

Maana yake ni kwamba hali ya ummah huu itaendelea kuwa njema na yenye heshima muda wa kuwa wanahifadhi Sunnah hii.

[1] al-Bukhaariy (1957) na Muslim (1098).

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tawjiyhaat wa Tanbiyhaat lil-Fataati al-Muslimah, uk. 33
  • Imechapishwa: 28/02/2026