32. Hii ndio shirki ambayo Allaah ametahadharisha nayo

na ukajua kumshirikisha Allaah ambako Allaah amekuzungumzia kwa kusema:

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ

“Hakika Allaah hasamehe kushirikishwa na kitu chochote na anasamehe yaliyo chini ya hayo kwa Amtakae.” (an-Nisaa´ 04 : 48)

MAELEZO

Bi maana shirki katika ´ibaadah na sio shirki ya kuitakidi ya kwamba kuna yeyote anayeumba, anayeruzuku na kuyaendesha mambo pamoja na Allaah. Shirki ambayo Allaah ametahadharisha nayo ni kule kuitakidi kuwa kuna yeyote anayestahiki ´ibaadah au kitu katika ´ibaadah pamoja na Allaah.

Shirki ni kumuomba Allaah pamoja na Allaah au kufanya kitu katika sampuli za ´ibaadah kwa asiyekuwa Allaah. Hii ndio shirki ambayo Allaah ameharamisha na Allaah akamharamishia mwenye nayo Pepo na akaeleza kuwa mwisho wake ni Motoni. Ni shirki inayoharibu matendo yote. Inahusiana na shirki katika uungu na sio shirki katika uola. Huu ni uzinduzi wa Shaykh (Rahimahu Allaah) ya kwamba kama ambavyo ni wajibu kuitambua Tawhiyd vivyo hivyo ni wajibu kuitambua shirki.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 48
  • Imechapishwa: 20/11/2016