98 – Ibn Abiy ´Awfaa (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kwamba: “Alikuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pindi anapoinua mgongo wake kutoka katika Rukuu´ basi anasema:
سَمِعَ اللَّهُ لِمَنْ حَمِدَهُ، اللَّهُمَّ رَبَّنَا لَكَ الْحَمْدُ ، مِلْءَ السَّمَاوَاتِ، وَمِلْءَ الْأَرْضِ، وَمِلْءَ مَا شِئْتَ مِنْ شَيْءٍ بَعْدُ
“Allaah amemsikia mwenye kumhimidi. “Ee Mola wetu, himdi zote njema ni Zako, zilizojaa mbingu, zilizojaa ardhi na zilizojaa vyote vile utakavyo baada yake.”
Imekuja katika upokezi mwingine:
اللَّهُمَّ لكَ الحَمْدُ مِلْءُ السَّماءِ، ومِلْءُ الأرْضِ، ومِلْءُ ما شِئْتَ مِن شيءٍ بَعْدُ اللَّهُمَّ طَهِّرْنِي بالثَّلْجِ والْبَرَدِ، والْماءِ البارِدِ اللَّهُمَّ طَهِّرْنِي مِنَ الذُّنُوبِ والْخَطايا، كما يُنَقَّى الثَّوْبُ الأبْيَضُ مِنَ الوَسَخِ
“Ee Allaah, himdi zote njema ni Zako, zilizojaa mbingu, zilizojaa ardhi na zilizojaa vyote vile utakavyo baada yake. Ee Allaah, nitakase kwa theluji, barafu na maji yenye baridi. Ee Allaah, nitakase na dhambi na makosa kama inavyotakasa nguo nyeupe kutokamana na uchafu.”[1]
Ameipokea Muslim.
99 – Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesimulia ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anaponyanyua kichwa chake kutoka katika Rukuu´ husema:
اللَّهُمَّ رَبَّنَا لَكَ الْحَمْدُ ، مِلْ السَّمَاوَاتِ، وَمِلْءَ الأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا ، وَمِلْءَ مَا شِئْتَ مِنْ شَيْءٍ بَعْدُ، أَهْلَ الثَّنَاءِ وَالْمَجْدِ، لَا مَانِعَ لِمَا أَعْطَيْتَ، وَلَا مُعْطِيَ لِمَا مَنَعْتَ ، وَلَا يَنْفَعُ ذَا الْجَدِّ مِنْكَ الْجَدُّ
“Ee Allaah, Mola wetu! Himdi zote njema ni Zako, zilizojaa mbingu, zilizojaa ardhi na vyote vilivyomo ndani yake na zilizojaa vyote vile utakavyo baada yake. Wewe unastahiki kusifiwa na kutukuzwa. Hakuna awezae kukizuia Ulichokitoa na wala kutoa ulichokizuia. Tajiri hanufaiki na utajiri wake mbele Yako.”[2]
Ameipokea Muslim.
MAELEZO
Katika Hadiyth hii kuna kupendeza kusema Dhikr hii baada ya kuinuka kutoka katika Rukuu´. Kilicho cha wajibu ni kusema:
رَبَّنَا وَلَكَ الْحَمْدُ
“Ee Mola wetu, himdi zote njema ni Zako.”
Chenye kuzidi juu yake kinapendeza. Miongoni mwa du´aa kamilifu zaidi iliyopokelewa ni kusema:

“Ee Allaah, Mola wetu! Himdi zote njema ni Zako, zilizojaa mbingu, zilizojaa ardhi na vyote vilivyomo ndani yake na zilizojaa vyote vile utakavyo baada yake. Wewe unastahiki kusifiwa na kutukuzwa, ni ukweli yale yaliyosemwa na mja, na sisi wote Kwako ni waja. Ee Allaah! Hakuna awezae kukizuia Ulichokitoa na wala kutoa ulichokizuia. Tajiri hanufaiki na utajiri wake mbele Yako.”
Kumekuja pia du´aa yenye kusema:
اللَّهُمَّ طَهِّرْنِي بِالثَّلْجِ وَالْبَرَدِ وَالْمَاءِ الْبَارِدِ اللَّهُمَّ طَهِّرْنِي مِنَ الذُّنُوبِ وَالْخَطَايَا ، كَمَا يُنَقَّى الثَّوْبُ الأَبْيَضُ مِنَ الْوَسَخ
“Ee Allaah, nitakase kwa theluji, barafu na maji yenye baridi. Ee Allaah, nitakase na dhambi na makosa kama inavyotakasa nguo nyeupe kutokamana na uchafu.”
Du´aa hii ni miongoni mwa zilizopwekeka katika Hadiyth hii Swahiyh.
[1] Muslim (477).
[2] Muslim (478).
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 100-102
- Imechapishwa: 03/11/2025

Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 100-102
Imechapishwa: 03/11/2025
https://firqatunnajia.com/32-duaa-ya-kuinuka-kutoka-katika-rukuu-iii/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket