96 – ar-Rifaa´ah bin Raafiy´ az-Zuraqiy´ amesimulia: “Siku moja tulikuwa tunaswali nyuma ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wakati aliponyanyua kichwa chake kutoka katika Rukuu´ akasema:

سَمِعَ اللَّهُ لِمَنْ حَمِدَهُ

“Allaah amemsikia mwenye kumhimidi.”

Bwana mmoja nyuma yake akasema:

رَبَّنَا وَلَكَ الْحَمْدُ، حَمْداً كَثيراً طَيِّباً مُبارَكاً فِيهِ

“Ee Mola wetu, himdi zote njema ni Zako, himdi nyingi, nzuri na zilizobarikiwa ndani yake.”

Alipomaliza akasema: “Ni nani aliyesema hivi?” Nikasema: “Mimi.” Akasema: “Nimeona Malaika thelathini na kitu wakishindana ni nani atakayekuwa wa kwanza kuyaandika.”[1]

Ameipokea al-Bukhaariy.

97 – Anas amesimulia: “Bwana mmoja alikuja akaingia ndani ya safu akiwa ni mwenye kuhema. Akasema:

الْحَمْدُ لِلَّهِ حَمْدًا كَثِيرًا طَيِّبًا مُبَارَكًا فِيهِ

“Himdi zote njema anastahiki Allaah, sifa nyingi, nzuri na zilizobarikiwa ndani yake.”

Wakati Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipomaliza swalah yake akasema: “Ni nani kati yenu aliyesema maneno haya?” Hakuna kitu kibaya. Akasema: “ Ni nani aliyesema hivi?” Hajasema kitu kibaya.” Bwana yule akasema: “Nilikuja na pumzi zikinienda mbio na hivyo ndio nikayasema.” Akasema: “Nimewaona Malaika kumi na wawili wakishindana ni nani katika yao atayapandisha.”[2]

Ameipokea Muslim.

MAELEZO

Faida tunayopata katika Hadiyth hii ni fadhilah za kumsifu Allaah na kwamba ni jambo linalomridhisha Allaah (´Azza wa Jall) na kwamba sifa hii inakuwa baada ya imamu kusema:

سَمِعَ اللَّهُ لِمَنْ حَمِدَهُ

“Allaah amemsikia mwenye kumhimidi.”

Kwa ajili hiyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema:

“Nimeona Malaika thelathini na kitu wakishindana ni nani atakayekuwa wa kwanza kuyaandika.”

Baada ya kumsikia mtu mmoja akisema:

رَبَّنَا وَلَكَ الْحَمْدُ، حَمْداً كَثيراً طَيِّباً مُبارَكاً فِيهِ

“Ee Mola wetu, himdi zote njema ni Zako, himdi nyingi, nzuri na zilizobarikiwa ndani yake.”

Katika Hadiyth hii kuna fadhilah za Dhikr tukufu. Kwa hivyo mtu anatakiwa kudumu nayo.

[1] al-Bukhaariy (799).

[2] Muslim (600).

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 99-100
  • Imechapishwa: 03/11/2025