95 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Imamu akisema:

سَمِعَ اللَّهُ لِمَنْ حَمِدَهُ

“Allaah amemsikia mwenye kumhimidi.”

Semeni:

اللَّهُمَّ رَبَّنَا لَكَ الْحَمْدُ

“Ee Allaah, Mola wetu, himdi zote njema ni Zako.”

Kwani ambaye maneno yake yataenda sambamba na maneno ya Malaika atasamehewa madhambi yake yaliyokwishatangulia.”[1]

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

MAELEZO

Katika Hadiyth imekuja ya kwamba maamuma anatakiwa kusema:

اللَّهُمَّ رَبَّنَا لَكَ الْحَمْدُ

“Ee Allaah, Mola wetu, himdi zote njema ni Zako.”

Pale imamu atakaposema:

سَمِعَ اللَّهُ لِمَنْ حَمِدَهُ

“Allaah amemsikia mwenye kumhimidi.”

Asikusanye kati ya mawili hayo. Ambaye anatakiwa kukusanya kati ya Tasmiy´ na Tahmiyd ni imamu na yule anayeswali peke yake.

Kumepokelewa matamshi manne juu ya Tahmiyd. Yote yanapatikana kwa al-Bukhaariy na Muslim:

1 –

ربنا ولك الحمد

“Mola wetu, na himdi zote njema ni Zako.”[2]

2 –

ربنا لك الحمد

“Mola wetu, himdi zote njema ni Zako.”[3]

3 –

اللهم ربنا ولك الحمد

“Ee Allaah, Mola wetu, na himdi zote njema ni Zako.”[4]

Maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

سَمِعَ اللَّهُ لِمَنْ حَمِدَهُ

“Allaah amemsikia mwenye kumhimidi.”

Bi maana Allaah amesikia maombi yao na akaitikia maombi ya wenye kumuhimidi. Maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

ربنا ولك الحمد

“Mola wetu, na himdi zote njema ni Zako.”

Bi maana tumekuomba, Mola wetu, tukakuhimidi na kukusifu. Ni Zako himdi zote njema, kwa kutuongoza, tunakuomba, ni Zako himdi zote njema kwa kutuongoza kukutambua na kukuomba.

[1] al-Bukhaariy (796) na Muslim (409).

[2] al-Bukhaariy (689) na Muslim (392).

[3] al-Bukhaariy (722).

[4] al-Bukhaariy (796).

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 98-99
  • Imechapishwa: 03/11/2025