94 – ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anaporukuu husema:

اللَّهُمَّ لَكَ رَكَعْتُ، وَبِكَ آمَنْتُ، وَلَكَ أَسْلَمْتُ، خَشَعَ لَكَ سَمْعِي، وَبَصَرِي، وَمُخِّي، وَعَظْمِي، وَعَصَبِي

“Ee Allaah! Kwako nimerukuu, Wewe nimekuamini, Kwako nimejisalimisha, umenyenyekea Kwako usikizi wangu, uoni wangu, ubongo wangu, mfupa wangu na hisia zangu.”

Na anaposujudu husema:

اللَّهُمَّ لَكَ سَجَدْتُ وَبِكَ آمَنْتُ، وَلَكَ أَسْلَمْتُ، سَجَدَ وَجْهِيَ لِلَّذِي خَلَقَهُ، وَصَوَّرَهُ، وَشَقَّ سَمْعَهُ وَبَصَرَهُ، تَبَارَكَ اللَّهُ أَحْسنُ الْخَالِقينَ

“Ee Allaah! Kwako nimesujudu, Wewe nimekuamini, Kwako nimejisalimisha, uso wangu umemsujudia Yule ambaye kaumba, akautia sura na akapasua usikizi wake na uoni wake. ametakasika Allaah, mbora wa waumbaji.”[1]

Ameipokea Muslim.

MAELEZO

Dhikr hii inasemwa katika swalah ya usiku. Kwa sababu swalah ya usiku imejengeka juu ya urefushaji. Kwa hivyo mswaliji atafanya kisomo kirefu, Rukuu´ ndefu na Sujuud ndefu.

[1] Muslim (771).

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 97
  • Imechapishwa: 03/11/2025