32. Anayopasa mfungaji kujiepusha nayo: Kutotumia dawa za tone za kutia puani

3 – Bora mtu aache kutumia zile dawa za kuweka puani ili zisije kuingia kooni mwake. Kwa sababu pua ni njia inayopitisha chakula.

Kuhusu matone kwenye macho na kwenye masikio na vivyo hivyo kupaka wanja kwenye macho, mfungaji kuchelewesha kuvitumia hivo mpaka wakati wa usiku ndio bora zaidi kwa sababu ya kutoka nje ya tofauti kwa sababu wapo wanazuoni wenye kuyakataza hayo. Ijapokuwa maoni ya sawa ni kwamba havifunguzi kwa kutokuwepo dalili zinazofahamisha hivo. Lakini bora mtu aache kufanya hivo kwa sababu ya kushika tahadhari zaidi juu ya ´ibaadah hii tukufu.

Swalah na amani zimwendee Mtume wa Allaah, kizazi chake na Maswahabah zake wote.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus fiy Ramadhwaan, uk. 50
  • Imechapishwa: 24/04/2023