31. Uwajibu wa kuitambua Tawhiyd kwa moyo na sio kwa ulimi pekee

Ukielewa yale niliyokwambia na moyo wako ukakinaika

MAELEZO

Ukielewa yale… – Ukitambua yale niliyokwambia juu ya tofauti kati ya Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah na Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah na ukaelewa kuwa washirikina walikubali Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah na wakapinga Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah hata hivyo haikuwaingiza katika Uislamu, wakauawa na zikahalalishwa damu na mali zao, ukiyaelewa mambo haya na moyo wako ukakinaika… na sio kukubali kwa kutamka peke yake kama yule mtu anayehifadhi maana hii na akaitekeleza katika mtihani ili aweze kufaulu na wakati huo huo akawa hakubaliani nayo ndani ya moyo wake na akayafahamu kikamilifu, jambo ambalo halitoshi. Ujuzi ni kule kutambua ndani ya moyo na sio kwenye ulimi peke yake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 47
  • Imechapishwa: 19/11/2016