Mlango huu ni wenye kuwafurahisha wale waliofikwa na misiba. Wao badala ya kuhuzunika, kulia, kujipiga mashavu, kurarua nguo na kuomboleza wanatakiwa watoe swadaqah, kuswali, kuleta du´aa, msamaha, kusoma Qur-aan, kuswali, kufunga na matendo mengine ya kheri kwa ajili ya wale maiti wao. Iwapo watajua kuwa matendo haya yanawafikia wale maiti au kupitia kwayo ima wakasamehe madhambi yao, zikanyanyuliwa daraja zao au yote mawili, watafurahi.

Mlango huu umejengwa juu ya kuwazawadia matendo mema maiti na wale watu waliohai. Tutataja maoni mbalimbali ya wanachuoni juu ya suala hili. Kuna sampuli ya matendo mema ambayo wanachuoni wameafikiana kuwafikia maiti. Kuna aina nyingine ya matendo ambayo wanachuoni wametofautiana juu ya kuwafikia wale maiti.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Muhammad al-Hanbaliy al-Manbajiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasliyatu Ahl-il-Maswaa-ib, uk. 177
  • Imechapishwa: 19/11/2016