Nimewauliza Jahmiyyah kwamba Allaah si amesema:

قُولُواْ آمَنَّا بِاللّهِ

”Semeni: “Tumemwamini Allaah… ”[1]

وَقُولُواْ لِلنَّاسِ حُسْناً

”… ongeeni na watu kwa uzuri… ”[2]

وَقُولُوا آمَنَّا بِالَّذِي أُنزِلَ إِلَيْنَا وَأُنزِلَ إِلَيْكُمْ

”… na semeni: ”Tumeyaamini ambayo yameteremshwa kwetu na yaliyoteremshwa kwenu… ”[3]

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ وَقُولُوا قَوْلًا سَدِيدًا

“Enyi mlioamini! Mcheni Allaah na semeni kauli ya kweli [ya sawasawa].”[4]

فَإِن تَوَلَّوْا فَقُولُوا اشْهَدُوا بِأَنَّا مُسْلِمُونَ

”Wakikengeuka; basi semeni: “Shuhudieni kwamba sisi ni waislamu.”[5]

وَقُلِ الْحَقُّ مِن رَّبِّكُمْ

”Sema: ”Hii ni haki kutoka kwa Mola wenu.”[6]

وَإِذَا جَاءَكَ الَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِآيَاتِنَا فَقُلْ سَلَامٌ عَلَيْكُمْ

”Wanapokujia wale wanaoamini Aayah Zetu, basi sema ”Amani iwe juu yenu!”[7]

Hatujamsikia Allaah akiamrisha kusema kuwa maneno Yake ni kiumbe.

Amesema (Ta´ala):

وَلاَ تَقُولُواْ ثَلاَثَةٌ انتَهُواْ خَيْرًا لَّكُمْ

”… na wala msiseme: ”Watatu.” Komeni ni kheri kwenu!”[8]

وَلَا تَقُولُوا لِمَنْ أَلْقَىٰ إِلَيْكُمُ السَّلَامَ لَسْتَ مُؤْمِنًا

”… na wala msimwambie anayekuamkieni kwa amani: ”Wewe si muumini”…”[9]

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَقُولُوا رَاعِنَا

”Enyi walioamini! Msiseme: ”Tutegemee sikio!”[10]

وَلَا تَقُولُوا لِمَن يُقْتَلُ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ أَمْوَاتٌ

”Wala msiseme waliouliwa katika Njia ya Allaah: ”Ni wafu.”[11]

وَلَا تَقُولَنَّ لِشَيْءٍ إِنِّي فَاعِلٌ ذَٰلِكَ غَدًا إِلَّا أَن يَشَاءَ اللَّـهُ

”Wala usiseme kamwe kwa jambo lolote lile: ”Nitalifanya hilo kesho” isipokuwa ”akitaka Allaah”.” [12]

إِمَّا يَبْلُغَنَّ عِندَكَ الْكِبَرَ أَحَدُهُمَا أَوْ كِلَاهُمَا فَلَا تَقُل لَّهُمَا أُفٍّ وَلَا تَنْهَرْهُمَا

”Kama mmoja wao akifikia uzee naye yuko pamoja nawe au wote wawili, basi usiwaambie: “Uff!” na wala usiwakemee… ”[13]

وَلَا تَدْعُ مَعَ اللَّـهِ إِلَـٰهًا آخَرَ

”… na wala usiombe pamoja na Allaah mwabudiwa mwingine.”[14]

وَلَا تَقْتُلُوا أَوْلَادَكُم مِّنْ إِمْلَاقٍ

“Wala msiwaue watoto wenu kutokana na umasikini.”[15]

وَلَا تَجْعَلْ يَدَكَ مَغْلُولَةً إِلَىٰ عُنُقِكَ

“Na wala usifanye mkono wako kama uliofungwa shingoni mwako [kama bakhili].”[16]

وَلَا تَقْتُلُوا النَّفْسَ الَّتِي حَرَّمَ اللَّـهُ إِلَّا بِالْحَقِّ

”… na wala msiue nafsi ambayo ameiharamisha Allaah isipokuwa kwa haki.”[17]

لَا تَقْرَبُوا مَالَ الْيَتِيمِ إِلَّا بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ

”Na wala msiikaribie mali ya yatima isipokuwa kwa njia bora.”[18]

وَلَا تَمْشِ فِي الْأَرْضِ مَرَحًا

”… na wala usitembee katika ardhi kwa majivuno!”[19]

Mfano wa hayo ndani ya Qur-aan ni mengi. Haya ni mambo ambayo Allaah amekataza. Wala hatujaona sehemu hata moja akikataza kusema kuwa Qur-aan ni maneno Yake.

Malaika wameyaita maneno ya Allaah kuwa ni maneno na hawakuyaita kuwa ni kiumbe. Amesema (Ta´ala):

حَتَّىٰ إِذَا فُزِّعَ عَن قُلُوبِهِمْ قَالُوا مَاذَا قَالَ رَبُّكُمْ

”Mpaka itakapoondolewa fazaiko nyoyoni mwao [baada ya kuzimia]; watasema [wakiulizana]: “Amesema nini Mola wenu?”[20]

Malaika hawakusikia sauti ya Wahy kati ya ´Iysaa na Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhimaa wa sallam), hapa katikati kulipita miaka kadhaa. Wakati Allaah alipomfunulia Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ndipo Malaika wakasikia sauti ya Wahy kama vile chuma kilichoanguka juu ya mwamba. Ndipo wakafikiri kuwa Qiyaamah kimesimama, wakaingiwa na khofu na wakaporomoka juu ya nyuso zao kusujudu. Hiyo ndio maana ya maneno Yake (Ta´ala):

حَتَّىٰ إِذَا فُزِّعَ عَن قُلُوبِهِمْ قَالُوا مَاذَا قَالَ رَبُّكُمْ

”Mpaka itakapoondolewa fazaiko nyoyoni mwao [baada ya kuzimia]; watasema [wakiulizana]: “Amesema nini Mola wenu?”

Pindi khofu inapoondoka kutoka nyoyoni mwao, ndipo Malaika huinua vichwa vyao na wakaulizana: ”Kipi alichosema Mola wenu?” Hawakuuliza: ”Kipi alichoumba Mola wenu?” Huu ni ubainifu kwa yule ambaye Allaah ametaka kumwongoza[21].

[1] 2:136

[2] 2:83

[3] 29:46

[4] 33:70

[5] 3:64

[6] 18:29

[7] 6:54

[8] 4:171

[9] 4:94

[10] 2:104

[11] 2:154

[12] 18:23-24

[13] 17:23-24

[14] 28:88

[15] 6:151

[16] 17:29

[17] 6:151

[18] 6:152

[19] 31:18

[20] 34:23

[21] Ibn ´Aqiyl al-Hanbaliy amesema:

”Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) ameandika kitabu kinachoitwa ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah wal-Qadariyyah.” (al-Aadaab ash-Shar´iyyah (1/274))

Ibn Taymiyyah amesema:

”Kama alivosema Imaam Ahmad katika kitabu chake ”ar-Radd ´alaaz-Zanaadiqah wal-Jahmiyyah.”  (Tafsiyr Suurat-il-Ikhlaasw, uk. 239)

Ibn Kathiyr amesema:

”… na hivo ndivo alivosema Ahmad bin Hanbal katika kitabu ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah” (Tafsiyr al-Qur-aan al-´Adhwiym (3/304))

Ibn Hajar al-´Asqalaaniy amesema:

”Amesema waziwazi Ahmad katika kitabu “ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah.” (Fath-ul-Baariy (13/598))

  • Mhusika: Imaam Ahmad bin Hanbal (afk. 241)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah, uk. 118-120
  • Imechapishwa: 23/04/2024