26. Tiba ya tatu ya talaka ambayo ni kuheshimiana, kupendana na kila mmoja kutambua haki zake

03 – Maisha yasimame juu ya heshima, nafasi, mahaba na mapenzi

Hali ya mke iwe kama ilivopokelewa katika Hadiyth:

”… ambao anapokasirika [yule mume] anakuja na kuweka mkono wake juu ya mkono wa mume wake na kusema: “Mimi leo sionji usingizi mpaka uridhie.“[1]

Hii ndio hali ya mke mwema. Ni mamoja yeye ndiye amedhulumu au amedhulumiwa.

Na hali ya mume iyakariri maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Muumini mwanaume asimchukie muumini mwanamke. Akichukia kutoka kwake tabia fulani basi ataridhia nyingine.”[2]

Ameipokea Ahmad na Muslim.

Vilevile amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Mbora wenu ni yule mbora wenu kwa famili yake na mimi ni mbora wenu kwa familia yangu.”[3]

Ibn Maajah na at-Tirmidhiy.

[1] al-Bayhaqiy katika ”Shu´ab-ul-Iymaan” (11/171) (8358).

[2] Muslim (1469), at-Tirmidhiy (3895) na Ibn Maajah (1977).

[3] at-Tirmidhiy (3895) na Ibn Maajah (1977). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh Ibn Maajah” (1608).

  • Mhusika: Shaykh Jamaal bin Furahyaan al-Haarithiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Twalaaq – asbaabuhu wa ´ilaajuh, uk. 41-42
  • Imechapishwa: 23/04/2024