Miongoni mwa alama za elimu yenye manufaa ni kwamba mwenye nayo anakuwa mwenye kuyakimbia zaidi maisha ya kidunia, khaswa mambo ya uongozi, umaarufu na sifa. Kujitenga kwake mbali na mambo hayo na kupambana kwake kuyaepuka kunajulisha elimu yake yenye manufaa. Atapotumbukia katika moja ya mambo hayo pasi na kukusudia na kutaka kwake, basi mtu huyo anakuwa na khofu kubwa sana kutokana na matokeo yake kwa vile anachelea isije kuwa adhabu ya Allaah. Ni kama ambavo Imaam Ahmad alikuwa anachelea hilo juu ya nafsi yake wakati liliposhuhurika jina lake na kupata sifa.

  • Mhusika: Imaam Zayn-ud-Diyn bin Rajab al-Hanbaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan Fadhwl ´Ilm-is-Salaf ´alaa ´Ilm-il-Khalaf, uk. 82
  • Imechapishwa: 29/09/2021