30. Kila anavokuwa mjuzi ndivo unavozidi unyenyekevu wake

al-Hasan amesema:

“Mwanachuoni ni yule mwenye kuipa kisogo dunia na ana shauku ya Aakhirah, mwenye utambuzi juu ya dini yake na daima anakuwa mwenye kumwabudu Mola wake.”

Amesema katika upokezi mwingine:

“Mwanachuoni ni yule asiyemuhusudi aliye juu yake, hawachezei shere walio chini yake na wala hachukui malipo kwa ajili ya kufunza elimu aliyofunzwa na Allaah.”

Mfano wa hayo yamepokelewa kutoka kwa Ibn ´Umar.

Kadri inavozidi elimu ya mtu mwenye elimu yenye manufaa, ndivo kunavyozidi kunyenyekea, khofu, kujisalimisha na kujidhalilisha kwake mbele ya Allaah. Wamesema baadhi ya Salaf:

“Inatakikana kwa mwanachuoni kuweka mchanga juu ya kichwa chake kwa ajili ya kumnyenyekea Mola wake.”

Hilo ni kwa sababu kila ambavo inazidi elimu na kumtambua kwake Mola Wake, ndivo inavyozidi khofu, mapenzi, kujidhalilisha na kujisalimisha kwake mbele Yake.

  • Mhusika: Imaam Zayn-ud-Diyn bin Rajab al-Hanbaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan Fadhwl ´Ilm-is-Salaf ´alaa ´Ilm-il-Khalaf, uk. 81-82
  • Imechapishwa: 29/09/2021