4- Mtumzima ambaye amefikia upeo wa kutokwa na akili na hawezi kupambanua mambo. Si lazima kwake kufunga wala kutolewa chakula kwa sababu ´ibaadah hazimlazimu kwa kutokuwa na uwezo wa kupambanua ambapo amefanana na mtoto kabla ya kuwa na uwezo wa kupambanua mambo. Ikiwa baadhi ya nyakati anakuwa na uwezo wa kupambanua mambo na wakati mwingine anaondokwa na akili basi ni lazima kwake kufunga katika kile kipindi anachoweza kupambanua mambo pasi na kile kipindi anachoondokwa na akili. Swalah ina hukumu moja kama swawm. Haimlazimu katika kile kipindi anachoondokwa na akili na inamlazimu katika kile kipindi anachoweza kupambanua mambo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majaalis Shahr Ramadhwaan, uk. 45
  • Imechapishwa: 22/04/2020