140 –Muusa bin Ismaa´iyl amesema: Hammaad ametuhadithia, kutoka kwa ´Aliy bin Zayd, kutoka kwa Yuusuf bin Mihraan, kutoka kwa Ibn ´Abbaas ambaye amesema kuhusu maneno Yake Allaah (Ta´ala):

وَيَوْمَ تَشَقَّقُ السَّمَاءُ بِالْغَمَامِ وَنُزِّلَ الْمَلَائِكَةُ تَنزِيلًا

”Na Siku itakayofunguka mbingu kwa mawingu na Malaika watateremshwa mteremsho mkubwa wa mfuatano.”[1]

 “Watashuka wakazi wa mbingu ya chini na watakuwa wengi zaidi kuliko wakazi wa ardhini katika majini na watu. Watasema wakazi wa ardhini: “Mola wetu yuko kati yenu?” Watasema: “Hapana, lakini Atakuja.” Kisha itapasuka mbingu ya pili… Kisha ipasuke mbingu ya saba. Watasema: “Mola wetu yuko kati yenu?” Watasema: “Hapana, lakini Atakuja.” Halafu baadaye Aje Allaah (´Azza wa Jall) na Malaika waliokurubishwa ambao ni wengi zaidi kuliko wakazi wa mbinguni na wakazi wa ardhini.”

Wameipokea kikosi kutoka kwa Hammaad.

141 – Muhammad bin Sa´d al-´Awfiy amesema: Baba yangu amenihadithia: Ami yangu al-Husayn bin al-Hasan bin ´Atwiyyah al-´Awfiy ametuhadithia: Baba yangu amenihadithia, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Ibn ´Abbaas ambaye amesema kuhusu maneno Yake Allaah (Ta´ala):

السَّمَاءُ مُنفَطِرٌ بِهِ ۚ كَانَ وَعْدُهُ مَفْعُولًا

”Mbingu zitapasuka hapo, ahadi Yake itatimizwa.”[2]

”Mbingu zitapasuka pindi ataposhuka Mwingi wa huruma (´Azza wa Jall.”[3]

142 – Ahmad bin Hanbal amesema katika kitabu chake “az-Zuhd”: Wakiy´ ametuhadithia: ´Aliy bin ´Aliy ametuhadithia: Nimemsikia al-Hasan akisema:

”Nimepata khabari kwamba waislamu mafukara wataingia Peponi miaka 400 kabla ya wale matajiri. Wengine watakuwa wamekaa kwa magoti yao ambapo wajiliwe na Mola (´Azza wa Jall) na aseme: ”Nyinyi mlikuwa mahakimu na watawala wa watu. Haja na matakwa Yangu yalikuwa kwenu nyinyi… Naapa kwa Allaah! Hesabu ni kali isipokuwa ile itakayofanywa wepesi na Allaah.”

143 – ´Uthmaan bin Sa´iyd ad-Daarimiy amesema:

”Maneno yake Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusu ushukaji wa Allaah sio ya kushangaza kama maneno Yake (Ta´ala):

هَلْ يَنظُرُونَ إِلَّا أَن يَأْتِيَهُمُ اللَّـهُ فِي ظُلَلٍ مِّنَ الْغَمَامِ وَالْمَلَائِكَةُ

”Je, wanangojea nini isipokuwa Allaah awajie katika vivuli vya mawingu pamoja na Malaika?”

na:

وَجَاءَ رَبُّكَ وَالْمَلَكُ صَفًّا صَفًّا

“… na atakapokuja Mola wako na Malaika safu kwa safu.”[4]

Mwenye kuweza hilo la kwanza analiweza pia hili la pili.”[5]

144 – Harb al-Karmaaniy amesema:

”Ishaaq bin Raahuuyah amenisomea: ”Allaah (Ta´ala) amejisifu Mwenyewe ndani ya Kitabu Chake kwa sifa ambazo viumbe hawana haja ya kumsifu zaidi ya hivyo. Miongoni mwa sifa hizo ni maneno Yake:

هَلْ يَنظُرُونَ إِلَّا أَن يَأْتِيَهُمُ اللَّـهُ فِي ظُلَلٍ مِّنَ الْغَمَامِ وَالْمَلَائِكَةُ

”Je, wanangojea nini isipokuwa Allaah awajie katika vivuli vya mawingu pamoja na Malaika?”

na:

وَتَرَى الْمَلَائِكَةَ حَافِّينَ مِنْ حَوْلِ الْعَرْشِ

”Utawaona Malaika wakizunguka pembezoni mwa ‘Arshi.”[6]

145 – Abu ´Umar bin ´Abdil-Wahhaab amesema: ´Abdullaah bin Ahmad bin Hanbal ametuhadithia: Ismaa´iyl bin Ahmad ametuhadithia: Nilimsomea Muhammad bin al-Qaasim: Nimemsikia Muhammad bin Aslam at-Twusiy akisema:

”Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:

هَلْ يَنظُرُونَ إِلَّا أَن يَأْتِيَهُمُ اللَّـهُ فِي ظُلَلٍ مِّنَ الْغَمَامِ وَالْمَلَائِكَةُ

”Je, wanangojea nini isipokuwa Allaah awajie katika vivuli vya mawingu pamoja na Malaika?”

na:

وَجَاءَ رَبُّكَ وَالْمَلَكُ صَفًّا صَفًّا

“… na takapokuja Mola wako na Malaika safu kwa safu.”[7]

Yule anayekadhibisha ushukaji basi amemkadhibisha Allaah (Ta´ala) na Mtume wa Allaah (Swalla Alalahu ´alayhi wa sallam).”

[1] 25:25

[2] 73:18

[3] Jaamiy´-ul-Bayaan (29/89).

[4] 89:22

[5] ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah, uk. 47

[6] 39:75

[7] 89:22

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy (afk. 748)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Arba´iyn fiy Swifaati Rabb-il-´Aalamiyn, uk. 145-150
  • Imechapishwa: 11/06/2024