30. Swalah ya anayejikohozakohoza, kupuliza na kulia

Swali 30: Ni yepi maoni yenu mtu kujikohozakohoza, kupuliza na kulia ndani ya swalah? Je, mambo hayo yanabatilisha swalah?

Jibu: Kujikohozakohoza, kupuliza na kulia yote hayo hayaharibu swalah. Hapana vibaya kwayo haja ikipelekea kufanya hivo. Inachukiza kuyafanya ikiwa ni pasi na haja. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alijikohozakohoza kumfanyia ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh) wakati alipombishia hodi na yeye alikuwa anaswali.

Kuhusu kulia ni jambo limesuniwa katika swalah na kwenginepo kukitokana na unyenyekevu na kumwelekea Allaah pasi na kujikakama. Imesihi kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa analia ndani ya swalah. Hayo vilevile yamesihi kutoka kwa Abu Bakr as-Swiddiyq, ´Umar al-Faaruuq (Radhiya Allaahu ´anhumaa) na jopo la wengine katika Maswaahabah na waliowafuata kwa wema.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Muhimmah, uk. 32-33
  • Imechapishwa: 22/08/2022