Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Khofu ni juu ya mpwekeshaji ambaye anapita katika njia bila ya kuwa na silaha.

MAELEZO

Khofu ya maadui wa Mitume iko kwa yule mpwekeshaji ambaye anapita katika njia pasi na kuwa na silaha. Hana elimu atayoitumia kama silaha. Katika hali hii kunachelea juu yake akajadiliwa na mmoja katika hawa washirikina akamtia hoja zake na baada ya hapo akaangamia. Kwa hiyo ni lazima kwa mtu awe na elimu anayoraddi kwayo utata na kumsambaratisha adui. Mwenye kujadili anahitajia mambo mawili:

1 – Athibitishe dalili ya maoni yake.

2 – Abatilishe dalili ya mpinzani wake.

Hakuna njia ya kufikia mambo hayo mawili, isipokuwa kwa kuwa na ujuzi wa ile haki aliyomo pamoja na kuwa na ujuzi wa ile batili aliyomo mpinzani wake. Ni lazima haya yapatikane ili aweze kusambaratisha hoja za yule mpinzani wake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 56
  • Imechapishwa: 04/11/2023