30. Kutokuwa kheri kwa wale ambao makafiri wajinga ni wajuzi zaidi wa Shahaadah kuliko yeye

Hakuna kheri kwa mtu ikiwa wajinga makafiri wanajua zaidi yake maana ya “hapana mungu isipokuwa Allaah”.

MAELEZO

Hakuna kheri yoyote kwa mtu anayedai Uislamu, sivyo tu bali anadai kuwa ni katika wanachuoni, na wakati huo huo akawa hajui maana ya ´hapana mungu isipokuwa Allaah` ilihali makafiri wa ki-Quraysh walifahamu na wakaelewa maana yake. Jambo ni la khatari na la kutia aibu.

Ni wajibu kwa waislamu wazinduke juu ya dini yao na wazingatie Da´wah ya Mtume wao (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wanatakiwa kuielewa dini yao uelewa wa sawa na waisimamishe juu ya misingi ilio salama katika ´Aqiydah ya Tawhiyd na wajitenge mbali na shirki na washirikina. Wasitosheke na kule kujiita tu ´waislamu` pamoja na kubaki katika ada na desturi zinazoenda kinyume. Inahusiana na kurudirudi ibara tupu zisizosaidia kitu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 46
  • Imechapishwa: 18/11/2016