Imaam Ibn Qudaamah (Rahimahu Allaah) amesema:

رَّضِيَ اللَّـهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ

”Allaah amewawia radhi nao wamemridhia.”[1]

MAELEZO

5 – Kuridhia. Kuridhia ni miongoni mwa sifa za Allaah zilizothibiti kwa Qur-aan, Sunnah na maafikiano ya Salaf. Allaah (Ta´ala) amesema:

رَّضِيَ اللَّـهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ

”Allaah amewawia radhi nao wamemridhia.”

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah anaridhia kwa mja kuwa anapokula mlo basi akamuhimidi kwacho au akanywa kinywaji basi akamuhimidi kwacho.”[2]

Ameipokea Muslim.

Salaf wameafikiana juu ya kuthibitisha Allaah (Ta´ala) kuridhia. Kwa hiyo ni lazima kumthibitishia nayo pasi na kupotosha, kukanusha, kuifanyia namna wala kuipigia mfano. Ni kuridhia kikweli ambako kunalingana na Allaah (Ta´ala).

Ahl-ut-Ta´twiyl wamefasiri kuwa ni thawabu. Tunawaraddi kwa yale yaliyokwishatangulia katika kanuni ya nne.

[1] 5:119

[2] Muslim (2734).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 53
  • Imechapishwa: 18/10/2022