Imaam Ibn Qudaamah (Rahimahu Allaah) amesema:

يُحِبُّهُمْ وَيُحِبُّونَهُ

“Atakaowapenda nao watampenda.”[1]

MAELEZO

6 – Kupenda. Kupenda ni miongoni mwa sifa za Allaah zilizothibiti kwa Qur-aan, Sunnah na maafikiano ya Salaf. Allaah (Ta´ala) amesema:

فَسَوْفَ يَأْتِي اللَّـهُ بِقَوْمٍ يُحِبُّهُمْ وَيُحِبُّونَهُ

”… basi Allaah atawaleta watu [badala yao] atakaowapenda nao watampenda.”

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema siku ya Khaybar:

“Kesho nitampa bendera mtu ambaye anampenda Allaah na Mtume Wake na Allaah Naye anampenda na Mtume Wake.”[2]

Kuna maafikiano juu yake.

Salaf wameafikiana juu ya kuthibitisha Allaah (Ta´ala) kupenda. Kwa hiyo ni lazima kumthibitishia nayo kikweli pasi na kupotosha, kukanusha, kuifanyia namna wala kuipigia mfano. Ni kupenda kikweli ambako kunalingana na Allaah (Ta´ala).

Ahl-ut-Ta´twiyl wamefasiri kuwa ni thawabu. Tunawaraddi kwa yale yaliyokwishatangulia katika kanuni ya nne.

[1] 05:54

[2] al-Bukhaariy (4210) na Muslim (2406).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 54
  • Imechapishwa: 18/10/2022