Imaam Ibn Qudaamah (Rahimahu Allaah) amesema:

Amesema (Subhaanah):

وَجَاءَ رَبُّكَ وَالْمَلَكُ صَفًّا صَفًّا

”Na atakapokuja Mola Wako na Malaika safu kwa safu.”[1]

هَلْ يَنظُرُونَ إِلَّا أَن يَأْتِيَهُمُ اللَّـهُ

”Je, wanangojea nini isipokuwa Allaah awajie.”[2]

MAELEZO

4 – Ujio. Kuja kwa Allaah kwa ajili ya kutoa hukumu kati ya waja siku ya Qiyaamah kumethibiti kwa Qur-aan, Sunnah na maafikiano ya Salaf. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَجَاءَ رَبُّكَ وَالْمَلَكُ صَفًّا صَفًّا

”Na atakapokuja Mola Wako na Malaika safu kwa safu.”

هَلْ يَنظُرُونَ إِلَّا أَن يَأْتِيَهُمُ اللَّـهُ

”Je, wanangojea nini isipokuwa Allaah awajie.”

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“… mpaka pale watapobaki isipokuwa wale wanaomwabudu Allaah ndipo atawajia Mola wa walimwengu.”[3]

Kuna maafikiano juu yake.

Salaf wameafikiana juu ya kuthibitisha kuja kwa Allaah (Ta´ala). Kwa hiyo ni lazima kumthibitishia nayo pasi na kupotosha, kukanusha, kufanyia namna wala kupigia mfano. Ni kuja kikweli ambako kunalingana na Allaah (Ta´ala).

Ahl-ut-Ta´twiyl wameifasiri kwamba ni kuja kwa amri Yake. Tunawaraddi kwa yale yaliyokwishatangulia katika kanuni ya nne.

[1] 89: 22

[2] 02:210

[3] al-Bukhaariy (7439) na Muslim (183).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 52
  • Imechapishwa: 18/10/2022