Allaah ametaja maneno Yake maeneo mengi ndani ya Qur-aan. Ameita kuwa ni maneno na kamwe hajawahi kuyaita kuwa ni kiumbe. Amesema (Ta´ala):

فَتَلَقَّىٰ آدَمُ مِن رَّبِّهِ كَلِمَاتٍ

“Halafu Aadam akapokea maneno.”[1]

أَفَتَطْمَعُونَ أَن يُؤْمِنُوا لَكُمْ وَقَدْ كَانَ فَرِيقٌ مِّنْهُمْ يَسْمَعُونَ كَلَامَ اللَّـهِ ثُمَّ يُحَرِّفُونَهُ مِن بَعْدِ مَا عَقَلُوهُ وَهُمْ يَعْلَمُونَ

”Je, mnatumai kwamba watakuaminini na hali lilikuwa kundi miongoni mwao linasikia Maneno ya Allaah kisha linayageuza baada ya kuyaelewa na hali wanajua?”[2]

وَلَمَّا جَاءَ مُوسَىٰ لِمِيقَاتِنَا وَكَلَّمَهُ رَبُّهُ

“Na alipokuja Muusa katika miadi Yetu na Mola wake akamsemesha.”[3]

يَا مُوسَىٰ إِنِّي اصْطَفَيْتُكَ عَلَى النَّاسِ بِرِسَالَاتِي وَبِكَلَامِي

”Ee Muusa! Hakika Mimi nimekuteua juu ya watu kwa Ujumbe na maneno Yangu.”[4]

وَكَلَّمَ اللَّـهُ مُوسَىٰ تَكْلِيمًا

”Na bila shaka Allaah alimzungumzisha Muusa maneno kihakika.”[5]

فَآمِنُوا بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ النَّبِيِّ الْأُمِّيِّ الَّذِي يُؤْمِنُ بِاللَّـهِ وَكَلِمَاتِهِ وَاتَّبِعُوهُ لَعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ

”Basi mwaminini Allaah na Mtume Wake, ambaye hajui kuandika wala kusoma, ambaye anamwamini Allaah na maneno Yake na mfuateni ili mpate kuongoka.”[6]

Allaah akatueleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akimuamini Allaah na maneno Yake Allaah. Amesema (Ta´ala) tena:

يُرِيدُونَ أَن يُبَدِّلُوا كَلَامَ اللَّـهِ

“Wanataka kubadilisha maneno ya Allaah.”[7]

قُل لَّوْ كَانَ الْبَحْرُ مِدَادًا لِّكَلِمَاتِ رَبِّي لَنَفِدَ الْبَحْرُ قَبْلَ أَن تَنفَدَ كَلِمَاتُ رَبِّي وَلَوْ جِئْنَا بِمِثْلِهِ مَدَدًا

“Sema: “Endapo bahari ingelikuwa ni wino wa [kuandika] maneno ya Mola wangu, basi ingelimalizika bahari kabla ya kumalizika maneno ya Mola wangu ijapo tungelileta mfano wake kujaza tena.”[8]

وَإِنْ أَحَدٌ مِّنَ الْمُشْرِكِينَ اسْتَجَارَكَ فَأَجِرْهُ حَتَّىٰ يَسْمَعَ كَلَامَ اللَّـهِ

“Endapo mmoja katika washirikina atakuomba umlinde, basi mlinde mpaka aweze kusikia maneno ya Allaah.”[9]

Hakusema ”mpaka aweze kusikia uumbaji wa Allaah”.

Aayah hizi ni kwa kiarabu kilicho wazi kabisa. Hakihitaji kufasiriwa, kwa sababu kiko wazi – na himdi zote njema ni stahiki ya Allaah[10].

[1] 2:37

[2] 2:75

[3] 7:143

[4] 7:144

[5] 4:164

[6] 7:158

[7] 48:15

[8] 18:109

[9] 9:6

[10] Ibn ´Aqiyl al-Hanbaliy amesema:

”Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) ameandika kitabu kinachoitwa ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah wal-Qadariyyah.” (al-Aadaab ash-Shar´iyyah (1/274))

Ibn Taymiyyah amesema:

”Kama alivosema Imaam Ahmad katika kitabu chake ”ar-Radd ´alaaz-Zanaadiqah wal-Jahmiyyah.”  (Tafsiyr Suurat-il-Ikhlaasw, uk. 239)

Ibn Kathiyr amesema:

”… na hivo ndivo alivosema Ahmad bin Hanbal katika kitabu ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah” (Tafsiyr al-Qur-aan al-´Adhwiym (3/304))

Ibn Hajar al-´Asqalaaniy amesema:

”Amesema waziwazi Ahmad katika kitabu “ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah.” (Fath-ul-Baariy (13/598))

  • Mhusika: Imaam Ahmad bin Hanbal (afk. 241)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah, uk. 117-118
  • Imechapishwa: 22/04/2024