30. Afanye nini mtu akitilia shaka ni lini alianza kupangusa na kumebaki muda kiasi gani?

Swali 30: Afanye nini mtu akitilia shaka ni lini alianza kupangusa na kumebaki muda kiasi gani?

Jibu: Katika hali hii ajengee juu ya yakini. Akitilia shaka kama alipangusa katika wakati wa swalah ya Dhuhr au swalah ya ´Aswr, basi ajaalie kuanza kuhesabu muda iwe ni ´Aswr. Kimsingi ni kutopangusa. Dalili ya kanuni hii ni kwamba mambo ni yenye kubaki kama yalivo na  msingi ni kule mtu kuwa hakupangusa. Kuna mtu alimshtakia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba anahisi kitu ndani ya swalah yake ambapo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamwambia:

“Asitoke mpaka asikie sauti au ahisi harufu.”[1]

[1] al-Bukhaariy (137) na Muslim (361).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Buhuuth wa Fataawaa fiyl-Mas´h ´alaal-Khuffayn, katika Majmuu´-ul-Fataawaa (11/176)
  • Imechapishwa: 06/05/2021