29. Msimamo wa Abu ´Ubaydah al-Jarraah kwa babake kafiri

Imesemekana kwamba Aayah hii imeteremka juu ya Abu ´Ubaydah bin al-Jarraah (Radhiya Allaahu ´anh) wakati alipouliwa baba yake siku ya vita vya Badr. Kwa sababu baba yake alikuwa juu ya ukafiri na alikuwa anataka kumuua mwanae Abu ´Ubaydah ambapo Abu ´Ubaydah yeye (Radhiya Allaahu ´anh)akawahi kumuua. Kwa sababu alikuwa ni adui wa Allaah na haikumzuia kwamba ni baba yake. Hilo halikumzuia kumuua kwa sababu ya kukasirika kwa ajili ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Maneno Yake (Ta´ala):

أُولَـٰئِكَ

”Hao.”

Bi maana wale ambao wanajiweka mbali kuwapenda na kujenga urafiki na wale wenye kumpinga Allaah na Mtume Wake. Maneno Yake (Ta´ala):

كَتَبَ فِي قُلُوبِهِمُ الْإِيمَانَ

”[Allaah] Amewaandikia katika nyoyo zao imani.”

Allaah amethibitisha na ameikita imani ndani ya mioyo yao. Maneno Yake (Ta´ala):

وَأَيَّدَهُم بِرُوحٍ مِّنْهُ ۖ وَيُدْخِلُهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ

“… na Akawatia nguvu kwa Roho kutoka Kwake na Atawaingiza kwenye mabustani yapitayo chini yake mito.”

Roho ndani ya Qur-aan ina maana nyingi. Kuna roho ambayo ni ile nafsi ambayo kwayo ndio kunapatikana uhai. Kuna roho kwa maana ya Wahy. Amesema (Ta´ala):

وَكَذَٰلِكَ أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ رُوحًا مِّنْ أَمْرِنَا

“Namna hiyo ndivyo Tulivyokuletea Roho kutokana na amri Yetu.”[1]

Roho ikiwa na maana ya Jibriyl. Yeye ni roho mtakatifu na roho mwaminifu. Amesema (Ta´ala):

قُلْ نَزَّلَهُ رُوحُ الْقُدُسِ مِن رَّبِّكَ بِالْحَقِّ لِيُثَبِّتَ الَّذِينَ آمَنُوا وَهُدًى وَبُشْرَىٰ لِلْمُسْلِمِينَ

“Sema: “Ameiteremsh Roho Mtakatifu kutoka kwa Mola wako kwa haki ili iwathibitishe wale walioamini na ni mwongozo na bishara njema kwa waislamu.”[2]

نَزَلَ بِهِ الرُّوحُ الْأَمِينُ

“Ameiteremsha Roho mwaminifu.”[3]

Roho, kama ilivyo katika Aayah hii, ikiwa na maana ya nguvu. Akawatia nguvu kwa roho kutoka Kwake ikiwa na maana ya nguvu kutoka Kwake (Subhaanahu wa Ta´ala). Nguvu ya imani duniani na Aakhirah:

وَيُدْخِلُهُمْ جَنَّاتٍ

“Atawaingiza kwenye mabustani… ”

Wingi wa Pepo. Maana ya Pepo kilugha ni bustani. Imeitwa kuwa ni Pepo kwa sababu imefunikwa na miti. Imesitiriwa na kufunikwa na miti iliyojaa. Kwa sababu Pepo ni vivuli, miti, mito, majumba na juu yake na paa yake ni ´Arshi ya Mwingi wa huruma (Subhaanahu wa Ta´ala). Maneno Yake (Ta´ala):

تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا

“… yapitayo chini yake mito, ni wenye kudumu humo.”

Bi maana ni wenye kubaki humo na hawatoondoka. Amesema (Ta´ala):

لَا يَبْغُونَ عَنْهَا حِوَلًا

“Hawatotaka kuihama.”[4]

Hawaogopi kufa na wala hawamwogopi yeyote kwamba atawaondoa na kuwafukuza kama ilivyo duniani. Mtu duniani anaweza kuwa katika kasiri lakini hata hivyo hasalimiki kutokamana na kifo na hivyo akatoka ndani yake. Vivyo hivyo hasalimiki kutokamana na maadui wenye kumshambulia na kumwondoa. Mtu duniani siku zote anakuwa ni mwenye khofu. Amesema (Ta´ala):

رَضِيَ اللَّـهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ

“Allaah Ameridhika nao, nao wameridhika Naye.”

Pindi walipowakasirikia jamaa zao wa karibu katika makafiri na wakawajengea uadui ndipo Allaah akawatunuku radhi kutoka Kwake (Subhaanahu wa Ta´ala) kama malipo kwao. Wamejawa na hasira dhidi ya jamaa zao wa karibu makafiri na wamejawa na radhi za Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Matokeo yake Allaah akaridhika nao nao wakaridhika Naye. Maneno Yake (Ta´ala):

أُولَـٰئِكَ حِزْبُ اللَّـهِ

“Hao ndio kundi la Allaah.”

Hao ndio kundi la Allaah. Kuhusu makafiri wao ni pote. Allaah (Ta´ala) amesema kuhusu wao:

لَّا تَجِدُ قَوْمًا يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ يُوَادُّونَ مَنْ حَادَّ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ وَلَوْ كَانُوا آبَاءَهُمْ أَوْ أَبْنَاءَهُمْ أَوْ إِخْوَانَهُمْ أَوْ عَشِيرَتَهُمْ ۚ أُولَـٰئِكَ كَتَبَ فِي قُلُوبِهِمُ الْإِيمَانَ وَأَيَّدَهُم بِرُوحٍ مِّنْهُ ۖ وَيُدْخِلُهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا ۚ رَضِيَ اللَّـهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ ۚ أُولَـٰئِكَ حِزْبُ اللَّـهِ ۚ أَلَا إِنَّ حِزْبَ اللَّـهِ هُمُ الْمُفْلِحُونَ

 “Hutopata watu wanaomuamini Allaah na Siku ya Mwisho kuwa wanawapenda wale wanaopinzana na Allaah na Mtume Wake, japo wakiwa ni baba zao, watoto wao, ndugu zao au jamaa zao. Hao [Allaah] Amewaandikia katika nyoyo zao imani na Akawatia nguvu kwa Roho kutoka Kwake, na Atawaingiza kwenye mabustani yapitayo chini yake mito, ni wenye kudumu humo. Allaah Ameridhika nao, nao wameridhika Naye. Hao ndio kundi la Allaah. Tanabahi! Hakika kundi la Allaah ndio lenye kufaulu.”[5]

أُولَـٰئِكَ حِزْبُ الشَّيْطَانِ

“Hao ndio kundi la shaytwaan.”[6]

Bi maana kundi na wasaidizi wa shaytwaan. Kuhusu watu hawa wao ni wasaidizi wa Mola.

[1] 42:52

[2] 42:193

[3] 26:103

[4] 18:108

[5] 58:22

[6] 58:19

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 64-66
  • Imechapishwa: 07/12/2020