29. Mjuzi mkubwa wa washirikina wa leo juu ya Shahaadah

Mjuzi katika wao anafikiria ya kwamba maana yake ni kwamba hakuna mwenye kuumba, wala mwenye kuruzuku, wala mwenye kuyaendesha mambo isipokuwa Allaah.

MAELEZO

Kama alivyotaja hayo Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah katika kitabu chake “Tadmuriyyah” na wengineo kuhusu wanachuoni wa falsafa ya kwamba ´mungu` kwa mujibu wao ni yule mwenye uwezo wa kuumba. Kwa msemo mwingine ni yule mwenye kuweza kuumba, kuruzuku, kuhuisha na kufisha na wanazijenga ´Aqiydah zao juu ya hili na wanaifasiri shahaadah kwa maana hii na wanafanya Tawhiyd ni kule kukubali Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah, jambo ambalo ni kosa. Ikiwa hii ndio hali ya wale wajuzi wao ni vipi wale wajinga? Haya hayakutokamana na mengine isipokuwa ni kule kutilia umuhimu mdogo kulingania katika Tawhiyd na kuwafuata kichwa mchunga mababa na mababu na kutosheka na ule Uislamu wa kujinasibisha. Inahusiana na madhumuni na malengo ya kidunia ambayo Allaah ndio anajua uhalisia wake pasi na kujua dini sahihi iliyoasisiwa na Tawhiyd ya kweli.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 45
  • Imechapishwa: 16/11/2016