29. Kipi kinachosomwa katika Sunnah ya ´Ishaa na Witr na baada ya Witr?

Swali: Kipi kinachosomwa katika Sunnah ya ´Ishaa na Witr na baada ya Witr?

Jibu: Katika Sunnah ya ´Ishaa hakukupokelewa kusoma Suurah maalum. Kuhusu katika swalah ya Witr inasuniwa kusoma Suurah “al-A´laa”, “al-Kaafiruun” na “al-Ikhlaasw”. Atapotoa salamu ya Witr atasema:

سبحان الملك القدوس, سبحان الملك القدوس, سبحان الملك القدوس

“Ametakasika Mfalme, Mtakatifu. Ametakasika Mfalme, Mtakatifu. Ametakasika Mfalme, Mtakatifu.”

Hayo ni kutokana na yale yaliyopokelewa na watano, isipokuwa at-Tirmidhiy, kupitia kwa Ubayy bin Ka´b (Radhiya Allaahu ´anh) aliyesimulia:

“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wa Allaah alikuwa akisoma katika Witr “al-A´laa”, “al-Kaafiruun” na “al-Ikhlaasw”.”

Ahmad na an-Nasaa´iy wamezidisha:

“Anapotoa salamu husema:

سبحان الملك القدوس, سبحان الملك القدوس, سبحان الملك القدوس

“Ametakasika Mfalme, Mtakatifu. Ametakasika Mfalme, Mtakatifu. Ametakasika Mfalme, Mtakatifu.”

Imekuja katika upokezi mwingine:

“Ile mara ya tatu akinyanyua sauti yake juu.”

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

´Abdur-Razzaaq ´Afiyfiy

´Abdullaah bin Ghudayyaan

Swaalih al-Fawzaan

´Abdul-´Aziyz Aalish-Shaykh

Bakr Abu Zayd

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Swalaat-it-Taraawiyh, uk. 31-32
  • Imechapishwa: 20/04/2022