Swali 28: Tunawaona baadhi ya waislamu wanapuuza kutekeleza swalah kipindi cha miezi ya mwaka. Unapofika mwezi wa Ramadhaan basi wanaharakisha kuswali, kufunga na kusoma Qur-aan. Ni vipi inakuwa swawm ya watu hawa na ni zipi nasaha zako?

Jibu: Funga ya watu hawa ni sahihi. Ni swawm yenye kutoka kwa watu wake stahiki na haikuchanganyikana na chenye kuiharibu. Kwa hivyo inakuwa sahihi. Lakini nasaha zangu kwa watu hawa wamche Allaah juu ya nafsi zao na wamwabudu Allaah kwa yale ambayo Allaah amewawajibishia wakati na maeneo yote. Hakika mtu hajui ni lini kitamjia kifo. Huenda wakasubiria mwezi wa Ramadhaan na usiwafikie. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) hakujaalia kwa ajili ya ´ibaadah Yake kipindi cha mtu kupumzika isipokuwa mpaka wakati wa kufa. Amesema (Ta´ala) amesema:

وَاعْبُدْ رَبَّكَ حَتَّىٰ يَأْتِيَكَ الْيَقِينُ

“Mwabudu Mola wako mpaka ikufikie yakini.”[1]

Bi maana mpaka kikufikie kifo ambacho ndio yakini.

[1] 15:99

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: 48 mas-alatu fiy Swiyaam, uk. 26-27
  • Imechapishwa: 21/04/2021