28. Salaf wakitahadharisha Bid´ah

Kuna mapokezi mengi yasiyohesabika kutoka kwa Salaf. Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema:

”Dini bora ni dini ya Muhammad. Uovu wa mambo ni yale yaliyozuliwa. Fuateni na wala msizue. Hakika hamtopotea muda wa kuwa mnafuata mapokezi. Mkitufuata, basi mtakuwa mmejishindia mbali sana. Mkienda kinyume nasi, basi mtakuwa mmepotea mbali upotevu wa sana. Hakika Ummah wowote ambao utazua ndani ya dini Bid´ah yoyote isipokuwa hunyanyua kutoka kwao njia ya uongofu kisha baada ya hapo kamwe hairudi kwao. Napendelea kuona moto unaowaka kando ya msikiti kuliko kuona Bid´ah isiyokuwa na mwenye kuibadilisha.”[1]

Mu´aadh bin Jabal (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

”Tahadharini na mambo yenye kuzuliwa. Hakika mambo yaliyozuliwa ni upotofu.”[2]

Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema:

”Jilazimiane na kushika msimamo, kuwafata viongozi na mapokezi na jiwekeni mbali na mambo ya uzushi.”[3]

Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema:

”Kila Bid´ah ni upotofu hata kama watu wataziona ni nzuri.”[4]

Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema:

”Hakika mambo yanayochukiza zaidi mbele ya Allaah (Ta´ala) ni Bid´ah.”[5]

Sufyaan ath-Thawriy amesema:

”Hakika Bid´ah ni zenye kupendeza zaidi kwa Ibliys kuliko maasi. Mtu hutubia kutokana na madhambi na hatubii kutokamana na Bid´ah.”[6]

Ibraahiym an-Nakha´iy (Rahimahu Allaah) amesema wakati alipoulizwa kuhusu matamanio:

“Allaahhakupatapo kuweka ndani yake chembe ya mbegu ya hardali ya kheri. Hakuna jambo isipokuwa lile la mwanzo.”[7]

Imaamash-Shaafi´iy (Rahimahu Allaah) amesema:

“Ni bora mtu akutane na Allaah akiwa na kila dhambi isiyokuwa shirki, kuliko kukutana Naye akiwa na kitu katika matamanio.”[8]

Imaam wa Ahl-us-Sunnah Ahmad bin Hanbal (Rahimahu Allaah) amesema:

“Tunaona kuwa misingi ya Sunnah ni kushikamana na yale waliyokuwemo Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kuwaigiliza na kuacha Bid´ahna kila Bid´ah ni upotofu.”[9]

[1] as-Sunnah, uk. 24, ya Muhammad bin Naswr.

[2] al-Ibaanah (1/39) ya IbnBattah.

[3]as-Sunnah, uk. 24, ya Muhammad bin Naswr.

[4]as-Sunnah, uk. 24, ya Muhammad bin Naswr, al-Laalakaa’iy (1/92) na al-Bayhaqiy katika ”al-Madkhal” (180).

[5] as-Sunan (4/316) ya al-Bayhaqiy.

[6]al-Laalakaa’iy (1/132).

[7]Hilyat-ul-Awliyaa’ (4/222) ya Abu Nu´aym.

[8] Sharh-us-Sunnah (1/271) ya al-Baghawiy.

[9] Twabaqaat-ul-Hanaabilah (1/241) ya Ibn Abiy Ya´laa.

  • Mhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas Aal ´Abdil-Kariym
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hujaj al-Qawiyyah ´alaa anna Wasaa-il-ad-Da´wah Tawqiyfiyyah, uk. 33-34
  • Imechapishwa: 15/05/2023