Amesema (Ta´ala):

وَالنَّجْمِ إِذَا هَوَى

“Naapa kwa nyota zinapotua!”[1]

Hapo ilikuwa pale ambapo Quraysh walipoituhumu Qur-aan kuwa ni mashairi, ngano za kale na mkanganyiko wa maneno. Aidha baadhi wakasema kuwa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameyazua mwenyewe na wengine wakadai kuwa kuna wanaomfunza. Ndipo Allaah akaapa kwa nyota zinapotua, bi maana Qur-aan inapoteremshwa, na akasema:

وَالنَّجْمِ إِذَا هَوَىٰ مَا ضَلَّ صَاحِبُكُمْ وَمَا غَوَىٰ

“Naapa kwa nyota zinapotua. Hakupotoka swahibu wenu na wala hakukosea.”[2]

Bi maana Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hakuizua Qur-aan hii kutoka kwake mwenyewe:

وَمَا يَنطِقُ عَنِ الْهَوَىٰ إِنْ هُوَ إِلَّا وَحْيٌ يُوحَىٰ

”Wala hatamki kwa matamanio yake – hayo si chochote isipokuwa ni Wahy unaofunuliwa.”[3]

Bi maana Qur-aan. Hapa akabatilisha ya kuwa Qur-aan iwe kitu kingine kisichokuwa Wahy. Kisha akasema:

عَلَّمَهُ شَدِيدُ الْقُوَى ذُو مِرَّةٍ فَاسْتَوَى وَهُوَ بِالْأُفُقِ الْأَعْلَى وَهُوَ بِالْأُفُقِ الْأَعْلَى ثُمَّ دَنَا فَتَدَلَّى فَكَانَ قَابَ قَوْسَيْنِ أَوْ أَدْنَى فَأَوْحَى إِلَى عَبْدِهِ مَا أَوْحَى

“ … Amemfunza mwenye nguvu madhubuti. Mwenye muonekano mzuri na akalingana sawasawa. Naye yuko juu kabisa katika upeo wa macho; kisha akakurubia na akashuka; kisha akawa kiasi cha umbali wa ncha mbili au karibu zaidi. Akamfunulia wahy mja Wake yale aliyomfunulia wahy.”[4]

Allaah akaiita Qur-aan kuwa ni Wahy na hakuiita kuwa ni kiumbe[5].

[1] 53:1

[2] 53:1-3

[3] 53:4

[4] 53:5-10

[5] Ibn ´Aqiyl al-Hanbaliy amesema:

”Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) ameandika kitabu kinachoitwa ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah wal-Qadariyyah.” (al-Aadaab ash-Shar´iyyah (1/274))

Ibn Taymiyyah amesema:

”Kama alivosema Imaam Ahmad katika kitabu chake ”ar-Radd ´alaaz-Zanaadiqah wal-Jahmiyyah.”  (Tafsiyr Suurat-il-Ikhlaasw, uk. 239)

Ibn Kathiyr amesema:

”… na hivo ndivo alivosema Ahmad bin Hanbal katika kitabu ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah” (Tafsiyr al-Qur-aan al-´Adhwiym (3/304))

Ibn Hajar al-´Asqalaaniy amesema:

”Amesema waziwazi Ahmad katika kitabu “ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah.” (Fath-ul-Baariy (13/598))

  • Mhusika: Imaam Ahmad bin Hanbal (afk. 241)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah, uk. 111-113
  • Imechapishwa: 22/04/2024