28. Ndio maana washirikina wa kale ni wajuzi zaidi kuliko waislamu wa madai wa hii leo

Ukishajua ya kwamba makafiri wajinga walijua hilo, jambo la kushangaza ni kwa yue anayedai Uislamu na yeye hajui maana ya neno hili jambo ambalo walikuwa wanalijua wajinga makafiri. Badala yake anafikiria ya kwamba maana yake ni kutamka herufi zake bila ya kuiamini moyoni kwa kitu katika maana yake.

MAELEZO

Haya ni katika mambo ya kushangaza kabisa ya kwamba makafiri wajinga na washirikina waliokuwa katika zama za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) walielewa ya kwamba maana ya neno hili ni kumtakasia ´ibaadah Allaah na kuacha kuabudu visivyokuwa Yeye. Kwa ajili hiyo ndio maana wakakataa kulitamka kwa kuchelea kuacha kuwaabudu waungu wao na wakashabikia batili yao

Ndio maana washirikina wa kale ni wajuzi zaidi kuliko waislamu wa madai wa leo

Wale wanaodai Uislamu hii leo hawaelewi ya kwamba maana ya neno hili ni kuacha kuyaabudu makaburi na badala yake kumtakasia ´ibaadah Allaah. Kwa ajili hiyo ndio maana utawaona wanalitamka na wakati huo huo wako katika shirki zao. Hawaoni kujigonga huku na kukusanya baina ya vitu viwili vilivyo kinyume. Makafiri wajinga wakawa ni wajuzi zaidi wa ´hapana mungu isipokuwa Allaah` kuliko wao. Huyu anayejidai Uislamu anadhani kuwa makusudio ya neno hili ni kulitamka peke yake bila ya kuamini maana yake. Matokeo yake utaona ni wenye kulikariri na wakati huo huo wanawaomba maiti na waliyomo ndani ya makaburi usiku na mchana.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 44
  • Imechapishwa: 13/11/2016