Swali: Ni ipi hukumu ya mwenye kuzembea akampenda mwalimu wake na kuyatanguliza maneno yake juu ya maneno ya Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?

Jibu: Haya ni maasi na ni kufuata kichwa mchunga. Akihalalisha hilo na akaona kuwa mwalimu wake ni mwenye kutangulizwa kabla ya Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anakufuru kufuru kubwa. Hayo ni pale atapohalalisha hilo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 41
  • Imechapishwa: 13/11/2016