55 – ´Abdullaah bin Ibraahiym al-Muqriy ametukhabarisha: Rajaa’ bin Swuhayb ametuhadithia: Ya´quub al-Hadhwramiy ametuhadithia: Shu´bah ametuhadithia… (ح) Ahmad bin ´Abdillaah bin al-Hasan al-´Adawiy ametuhadithia huko Misri: Mu´aadh bin al-Muthannaa, ambaye tamko ni lake, ametuhadithia: Abul-Waliyd ametuhadithia: Shu´bah ametuhadithia, kutoka kwa Abu Ishaaq, kutoka kwa Abul-Ahwasw, kutoka kwa baba yake, ambaye amesimulia:

”Alimjilia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambaye akamwambia: ”Sehemu ya chini ya mkono wa Allaah ni yenye nguvu zaidi kuliko sehemu yako ya chini ya mkono, na kisu cha Allaah ni chenye makali zaidi kuliko kisu chako.”[1]

56 – ´Abdul-´Aziyz bin Sahl ad-Dabbaas ametukhabarisha huko Makkah: Muhammad bin al-Hasan al-Khiraqiy al-Baghdaadiy ametuhadithia: Mahfuudhw ametuhadithia, kutoka kwa Abu Tawbah, kutoka kwa ´Abdur-Razzaaq, kutoka kwa Ma´mar, kutoka kwa az-Zuhriy, kutoka kwa Ibn-ul-Musayyab, kutoka kwa Abu Hurayrah, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambaye amesema:

”Allaah (´Azza wa Jall) hushuka katika mbingu ya chini. Kwenye kila mbingu yuko na kiti. Anaposhuka kwenye mbingu ya chini huketi juu ya kiti Chake, akanyoosha sehemu Zake za mkono wa chini na akasema: ”Ni nani ambaye atamkopesha asiye masikini wala dhalimu? Ni nani ambaye ataniomba msamaha Nimsamehe? Ni nani ambaye atatunia Nimpokelee tawbah yake?” Alfajiri inapoingia basi Hupanda juu na kuketi juu ya kiti Chake.”[2]

Namna hii amepokea Mahfuudhw, kutoka kwa Abu Tawbah, kutoka kwa ´Abdur-Razzaaq. Asili yake imepokelewa na Sa´iyd bin al-Musayyab pasi na Swahabah kwenye cheni ya wapokezi.

57 – Muhammad bin ´Abdil-Jabbaar ametukhabarisha huko Misri: ar-Rabiy´ bin Sulaymaan ametuhadithia: Ibn Wahb ametuhadithia: Usaamah bin Yaziyd ametuhadithia, kutoka kwa Abu Haazim, kutoka kwa Ibn ´Umar, ambaye ameeleza:

”Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa juu ya mimbari akiwakhutubia watu akasema: ”al-Jabbaar atazichukua mbingu Zake na adhi na kuziweka kwenye kiganja Chake cha mkono, atazifanya namna hii, kama ambavo kijana anaufanya mpira, na kusema: ”Mimi ni Allaah, Mmoja! Mimi ni Allaah, Mshindi!”

58 – ´Abdullaah bin Ja´far al-Baghdaadiy ametukhabarisha huko Misri: Haashim bin Yuunus ametuhadithia: Abu Swaalih ametuhadithia, kutoka kwa Mu´aawiyah bin Swaalih, kutoka kwa ´Umar bin ´Amr, kutoka kwa baadhi ya watu wa Shaam, ambao wamesema:

”Mola (´Azza wa Jall) alichukua lulu na kuiweka kwenye kiganja Chake, kisha Akaikumbatia baina ya viganja Vyake. Kisha Akaipanda katikati ya Pepo na kuiambia: ”Mea mpaka…radhi Zangu.” Ikafanya hivo. Ilipomea, ikaanza kububujika kutoka kwenye mizizi yake mito ya Pepo. Nayo ni Twubaa.”[3]

59 – Ahmad bin Muhammad bin Ziyaad ametukhabarisha: Ahmad bin Muhammad as-Swaydalaaniy al-Baghdaadiy ametuhadithia: Sa´iyd, yaani Ibn ´Aamir, ametuhadithia: Shu´bah ametuhadithia, kutoka kwa Thaabit, kutoka kwa Anas, ambaye amesema kuhusiana na maneno Yake (´Azza wa Jall):

فَلَمَّا تَجَلَّىٰ رَبُّهُ لِلْجَبَلِ جَعَلَهُ دَكًّا

“Basi Mola wako alipojidhihirisha katika jabali, akalifanya livurugike kuwa vumbi.”[4]

Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Alionyesha kidole Chake kidogo. Kutokana na mwanga wake ukapasukapasuka.”[5]

60 – Ahmad bin Ziyaad ametuhadithia ametuhadithia mfano wake: Ahmad bin Muhammad as-Swaydalaaniy ametuhadithia: Ishaaq bin Abiy Ishaaq ametuhadithia: Daawuud, yaani Ibn-uz-Zibriqaan[6], ametuhadithia: Shu´bah ametuhadithia, kutoka kwa Qataadah, kutoka kwa Anas, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambaye amesema:

”Mlima ulikuwa juu ya ardhi.”

Hadiyth kama hiyo imepokelewa na  Muhammad bin Sawaa’ kutoka kwa Sa´iyd bin Abiy ´Aruubah, kutoka kwa Qataadah, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Zote mbili zimepokelewa kupitia kwa Shu´bah, ngeni na kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

[1] Ahmad (3/473). Cheni ya wapokezi ni Swahiyh kwa mujibu wa Shu´ayb al-Arnaa’uut.

[2] Mahfuudhw bin Abiy Tawbah alimsikia ´Abdur-Razzaaq. Ahmad alimdhoofisha vibaya na kusema:

”Alikuwa nasi Yemen. Hakuwa anaandika.”

Ibn Hajar amesema:

”Alikuwa akiitwa Mahfuudhw bin al-Fadhl. Amesimulia kutoka kwa Ma´n, Dhamrah na Rabiy´ah. Alisimulia kutoka kwa al-Qaadhwiy Ismaa´iyl na ´Umar bin Ayyuub as-Saqatwiy. Hakuwa mwenye kuachwa.”

al-´Uqayliy amemtaja katika “adh-Dhwu´afaa’”. Alifariki mwaka wa 237. Tazama “Lisaan-ul-Miyzaan” (5/19).

[3] Katika cheni ya wapokezi kuna ujinga, nao ni baadhi ya watu wa Shaam.

[4] 7:143

[5] at-Tirmidhiy (3074), ambaye amesema kuwa ni nzuri, ngeni na Swahiyh. Swahiyh kwa mujibu wa Albaaniy katika “Swahiyh Sunan at-Tirmidhiy” (3074).

[6] ar-Ruqaashiy al-Baswriy. Ibn Hajar amesema juu yake:

“Mwenye kuachwa.” (Taqriyb-ut-Taqriyb (1/231))

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Ishaaq bin Mandah (afk. 395)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah, uk. 80-82
  • Imechapishwa: 17/06/2026
  • Taaliki: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy