27. Kila mmoja amerahisishiwa kile alichoumbiwa

Mengine yanayofahamisha Mkono na Kiganja cha mkono

54 – ´Abdur-Rahmaan bin Yahyaa bin Mandah na ´Abdullaah bin Ibraahiym wametukhabarisha: Ahmad bin al-Furaat ametuhadithia: ´Abdullaah bin Swaalih ametuzindua: Mu´aawiyah bin Swaalih ametuhadithia, kutoka kwa Raashid bin Sa´d, kutoka kwa ´Abdur-Rahmaan bin Qataadah, kutoka kwa Hishaam bin Hakiym, ambaye amesimulia kuwa bwana mmoja amesema:

”Ee Mtume wa Allaah! Tuanze matendo au hukumu imeshaamuliwa?” Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: ”Allaah amechukua katika wana wa Aadam kutoka migongoni mwao kizazi chao na akawashuhudisha juu ya nafsi zao. Kisha akawatawanya kwenye kiganja Chake na akasema: “Hawa wataingia Peponi na hawa wataingia Motoni.” Watu wa Peponi wamerahisishiwa kufanya matendo ya watu wa Peponi na watu wa Motoni wamerahisishiwa kufanya matendo ya watu wa Motoni.”

Kuna wengi wamepokea Hadiyth hii kutoka kwa Mu´aawiyah bin Swaalih bila ya kutaja tamko lisemalo:

”Kisha akawatawanya kwenye kiganja Chake… “

az-Zubaydiy ameisimulia kutoka kwa Raashid kwa tamko lisemalo “kwenye kiganja Chake”. Miongoni mwa walioipokea ni ´Abdullaah bin Wahb, Ma´n bin ´Iysaa al-Qazzaaz na wengineo. Tumekhabarishwa hilo na ´Aliy bin al-´Abbaas at-Twahhaan al-Miswriy: Ja´far bin Sulaymaan an-Nawfaliy ametuhadithia: Ibraahiym bin al-Mundhir al-Haraaniy: Ma´n bin ´Iysaa ametuhadithia, kutoka kwa Mu´aawiyah bin Swaalih.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Ishaaq bin Mandah (afk. 395)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah, uk. 78-79
  • Imechapishwa: 17/06/2026
  • Taaliki: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy