Masimulizi mengine yanayofahamisha maneno Yake (´Azza wa Jall):

مَا مَنَعَكَ أَن تَسْجُدَ لِمَا خَلَقْتُ بِيَدَيَّ

”Kipi kilichokuzuia usimsujudie Niliyemuumba kwa mikono Yangu?”[1]

51 – Muhammad bin Ibraahiym bin ´Abdil-Malik al-Qurashiy ametukhabarisha: Ahmad bin Ibraahiym al-Busriy ametuhadithia: Abut-Twaahir Ahmad bin ´Amr ametuhadithia: Mjomba wangu ´Abdul-Hamiyd ametuhadithia: Yahyaa bin Ayyuub ametuhadithia, kutoka kwa Daawuud bin Abiy Hind, kutoka kwa Anas bin Maalik, ambaye amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Allaah (Jalla wa ´Azz) ameumba Firdaws kwa mkono Wake na akamharamishia nayo kila mshirikina na chapombe.”

52 – Ahmad bin Salamah al-Mu-addib ametukhabarisha huko Misri: Abuz-Zinbaa´ ametuhadithia: Sa´iyd bin ´Ufayr ametuhadithia: Yahyaa bin Ayyuub ametuhadithia, kutoka kwa Khaalid bin Yaziyd, kutoka kwa Sa´iyd bin Abiy Hilaal, kutoka kwa Anas bin Maalik, ambaye ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Allaah (Jalla wa ´Azz) ameumba Firdaws kwa mkono Wake na akamharamishia nayo kila mshirikina na chapombe.”

53 – Ahmad bin Muhammad bin ´Amr bin Abaan ametukhabarisha: ´Abdullaah bin Ahmad bin Hanbal ametuhadithia: Baba yangu ametuhadithia: Yahyaa bin Sa´iyd ametuhadithia, kutoka kwa Abu ´Ajlaan: Nimemsikia baba yangu akisimulia kutoka kwa Abu Hurayrah, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambaye amesema:

“Wakati Allaah (´Azza wa Jall) alipoumba viumbe alijifaradhishia Mwenyewe kwa mkono Wake: ”Hakika huruma Yangu inashinda ghadhabu Zangu.”[2]

Kuna wengi ambao wamesimulia Hadiyth hii kutoka kwa Abu Hurayrah, hata hivyo Ibn ´Ajlaan pekee ndiye ambaye amesimulia jumla isemayo “alijifaradhishia Mwenyewe kwa mkono Wake”.

[1] 38:75

[2] al-Bukhaariy (7554) na Muslim (2751).

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Ishaaq bin Mandah (afk. 395)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah, uk. 77-78
  • Imechapishwa: 17/06/2026
  • Taaliki: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy