25. Swadaqah inakuwa kwenye kiganja cha Mwingi wa rehema

50 – Muhammad bin Ya´quub bin Yuusuf bin al-Akhram ametukhabarisha huko Neyshabur: Muhammad bin Nu´aym ametuhadithia… (ح) Muhammad bin ´Abdillaah bin Abiy Rajaa’ ametuhadithia: Muusa bin Haaruun ametuhadithia: Qutaybah ametuhadithia: al-Layth ametuhadithia, kutoka kwa Sa´iyd bin Abiy Sa´iyd bin Yasaar, ambaye amemsikia Abu Hurayrah akisimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Hakika swadaqah hukua kwenye kiganja cha Mwingi wa huruma (´Azza wa Jall), mpaka inakuwa kubwa kuliko mlima, kama anavyolea mmoja wenu kitekli chake.”[1]

Hadiyth hii imethibiti kwa maafikiano.

[1] al-Bukhaariy (7430) na Muslim (702).

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Ishaaq bin Mandah (afk. 395)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah, uk. 76-77
  • Imechapishwa: 17/06/2026
  • Taaliki: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy