28. Mpwekeshaji ambaye si msomi anawashinda wanachuoni elfu wa washirikina

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Mtu ambaye si msomi katika wapwekeshaji [watu wa Tawhiyd] anashinda watu elfu katika wanachuoni wa washirikina. Kama alivyosema Allaah (Ta´ala):

وَإِنَّ جُندَنَا لَهُمُ الْغَالِبُونَ

“Na kwamba hakika jeshi Letu ndilo litakaloshinda.” (37:173)

MAELEZO

Shaykh (Rahimahu Allaah) amesema kuwa mpwekeshaji anawashinda wanachuoni elfu wa washirikina. Ametumia dalili maneno Yake (Ta´ala):

وَإِنَّ جُندَنَا لَهُمُ الْغَالِبُونَ

“Na kwamba hakika jeshi Letu ndilo litakaloshinda.”

Mpwekeshaji ambaye si msomi ni yule anayethibitisha aina zote tatu za Tawhiyd; Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah, Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah na Tawhiyd al-Asmaa´ was-Swifaat. Mtu kama huyo anawashinda wanachuoni elfu wa wanachuoni wa washirikina, kwa sababu wanachuoni wa washirikina wanathibitisha Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah peke yake. Tawhiyd sampuli hii ni pungufu na kiukweli sio aina ya Tawhiyd. Dalili ya hilo ni kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwapiga vita washirikina hawa ambao walikuwa wakithibitisha Tawhiyd aina hii. Tawhiyd hii haikuwafaa kitu na haikukinga damu na mali zao. Upande mwingine mpwekeshaji ambaye si msomi anathibitisha aina zote tatu za Tawhiyd na kwa ajili hiyo yeye ni bora kuliko watu hawa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 50
  • Imechapishwa: 04/11/2023