Imaam Ibn Qudaamah (Rahimahu Allaah) amesema:

Allaah (Ta´ala) amesema akielezea kuhusu ´Iysaa (´alayhis-Salaam) ya kwamba atasema:

تَعْلَمُ مَا فِي نَفْسِي وَلَا أَعْلَمُ مَا فِي نَفْسِكَ

”Unayajua yale yote yaliyomo katika nafsi yangu na wala mimi sijui yale yaliyomo katika nafsi Yako.”[1]

MAELEZO

3 – Nafsi. Nafsi imethibiti kwa Allaah kwa Qur-aan, Sunnah na maafikiano ya Salaf. Allaah (Ta´ala) amesema:

كَتَبَ رَبُّكُمْ عَلَىٰ نَفْسِهِ الرَّحْمَةَ

”Mola wenu amekidhia juu ya Nafsi Yake rehema.”[2]

Amesema kuhusu ´Iysaa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuwa amesema:

تَعْلَمُ مَا فِي نَفْسِي وَلَا أَعْلَمُ مَا فِي نَفْسِكَ

”Unayajua yale yote yaliyomo katika nafsi yangu na wala mimi sijui yale yaliyomo katika nafsi Yako.”

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

سُبْحَانَ الله وَبِحَمْدِهِ عَدَدَ خَلْقِهِ وَرِضَا نَفْسِهِ وَزِنَةَ عَرْشِةِ وَمِدَادَ كَلِمَاتِه

”Allaah ametakasika kutokamana na mapungufu yote na himdi zote njema ni Zake kwa idadi ya viumbe Wake, radhi Yake, uzito wa ´Arshi Yake na wino wa maneno Yake.”[3]

Ameipokea Muslim.

Salaf wameafikiana juu ya kumthibitishia Allaah nafsi kwa njia inayolingana Naye. Kwa hiyo ni lazima kumthibitishia nayo pasi na kupotosha, kukanusha, kuufanyia namna wala kuupigia mfano.

[1] 05:116

[2] 06:54

[3] Muslim (2726).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 51
  • Imechapishwa: 17/10/2022