Njia ambazo imepokelewa sifa ya mikono miwili na namna ya kuioanisha:

1 – Kutajwa kwa njia ya umoja. Amesema (Ta´ala):

تَبَارَكَ الَّذِي بِيَدِهِ الْمُلْكُ

“Amebarikika Ambaye mkononi Mwake umo ufalme.”[1]

2 – Kutajwa kwa njia ya uwili. Amesema (Ta´ala):

بَلْ يَدَاهُ مَبْسُوطَتَانِ

“Bali mikono Yake imekunjuliwa.”[2]

3 – Kutajwa kwa njia ya wingi. Amesema (Ta´ala):

أَوَلَمْ يَرَوْا أَنَّا خَلَقْنَا لَهُمْ مِمَّا عَمِلَتْ أَيْدِينَا أَنْعَامًا

“Je, hawaoni kwamba Sisi tumewaumbia kutokana na yale iliyofanya mikono Yetu wanyama wa mifugo.”[3]

Namna ya kuoanisha njia hizi ni sisi kusema kuwa mkono wa kwanza ni moja iliyoegemezewa. Kwa hiyo inakusanya kila mkono uliyothibiti kwa Allaah. Hilo halipingani na mbili. Kuhusu wingi ni kwa ajili ya matukuzo na si uhakika wa idadi ambayo ni idadi isiyopungua chini ya tatu. Kwa hiyo itakuwa jambo hilo halipingani na mbili. Licha ya kwamba imesemekana kuwa uchache wa wingi ni mbili. Kwa hiyo ikichukuliwa wingi juu ya uchache wake basi hakuna kupingana kabisa kati hiyo wingi na idadi ya mbili[4].

[1] 67:01

[2] 05:64

[3] 36:71

[4] Faida!

Haafidhw amesema alipokuwa anazungumzia tamko la Muslim na upokezi wake na kwamba imetokea badala ya mkono wa Allaah ikaja ”mkono wa kuume wa Allaah”:

”Hapa anakosolewa ambaye amefasiri mkono kuwa ni neema na aliyekwenda mbali zaidi na usawa ni yule ambaye ameifasiri mikono kuwa ni hazina na akasema mkono kwa njia isiyofungamana kuwa ni hazina ili apate kupindisha.” (Fath-ul-Baariy 13/395)).

Hapa kuna dalili kuwa Haafidhw anawaraddi Mu´awwilah.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 50
  • Imechapishwa: 17/10/2022