Imaam Ibn Qudaamah (Rahimahu Allaah) amesema:

بَلْ يَدَاهُ مَبْسُوطَتَانِ

”Bali mikono Yake imefumbuliwa.”[1]

MAELEZO

2 – Mikono miwili. Mikono miwili ni miongoni mwa sifa za Allaah zilizothibiti kwa Qur-aan, Sunnah na maafikiano ya Salaf. Allaah (Ta´ala) amesema:

بَلْ يَدَاهُ مَبْسُوطَتَانِ

”Bali mikono Yake imefumbuliwa.”[2]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mkono wa kuume wa Allaah umejaa. Haupungui kwa kutoa usiku na mchana.” Mpaka aliposema: “Kwa mkono Wake mwingine anakamata; anainua na anashusha.”[3]

Ameipokea Muslim na al-Bukhaariy amepokea maana yake.

Salaf wameafikiana juu ya kumthibitishia Allaah (Ta´ala) mikono miwili. Kwa hiyo ni lazima kumthibitishia nayo pasi na kupotosha, kukanusha, kuifanyia namna wala kuipigia mfano. Ni mikono miwili ya Allaah ya kikweli inayolingana Naye.

Ahl-ut-Ta´twiyl wameifasiri kuwa ni neema, uwezo na mfano wake. Tunawaraddi kwa yale yaliyokwishatangulia katika kanuni ya nne. Kuna njia nyingine ya nne; nayo ni kwamba katika mtiririko wa maneno kuna yanayozuia kabisa kufasiri namna hiyo. Amesema (Ta´ala):

قَالَ يَا إِبْلِيسُ مَا مَنَعَكَ أَن تَسْجُدَ لِمَا خَلَقْتُ بِيَدَيَّ

”Kipi kilichokuzuia usimsujudie Niliyemuumba kwa mikono Yangu?”[4]

Maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Kwa mkono Wake mwingine anakamata; anainua na anashusha.”

[1] 05:64

[2] 05:64

[3] Muslim (993) na al-Bukhaariy (4684).

[4] 38:75

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 49-50
  • Imechapishwa: 17/10/2022