28. Dalili ya kumi na tano kutoka katika Sunnah juu ya mikono ya Allaah

29- Abu Hurayrah amepokea tena kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): al-Bayhaqiy ameipokea kutoka kwa al-Haakim: Muhammad bin Ya´quub ametuhadithia: Bakkaar bin Qutaybah ametuhadithia Misri: Swafwaan bin ´Iysaa ametuhadithia: al-Haarith bin ´Abdir-Rahmaan bin Abu Dhubaab ametuhadithia, kutoka kwa al-Maqbariy, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Abu Hurayrah:

“Allaah akamwambia na mikono Yake yote miwili ilikuwa imefumbuliwa: “Chagua utakao… “[1]

[1] al-Haakim ambaye amesema:

”Hadiyth ni Swahiyh juu ya masharti ya Muslim.” (al-Mustadrak (1/64))

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ithbaat-ul-Yad li-Laah Swifatan min Swifwaatih, uk. 26
  • Imechapishwa: 24/07/2019