29. Dalili ya kumi na sita kutoka katika Sunnah juu ya mikono ya Allaah

30- Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Aadam na Muusa walihojiana. Muusa akamwambia: “Wewe ndiye baba yetu. Ulisababisha khasara kwetu na tukatolewa Peponi.” Aadam akasema: “Muusa! Allaah (´Azza wa Jall) alikuteua kwa maneno Yake na akakuandikia Tawraat kwa mkono Wake. Je, unanilaumu kwa kitu ambacho Allaah alikuwa tayari ameshanikadiria miaka 40 kabla ya kuniumba?” Aadam akamshinda Muusaa. Aadam akamshinda Muusaa. Aadam akamshinda Muusaa.”[1]

[1] al-Bukhaariy (6614) na Muslim (2652).

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ithbaat-ul-Yad li-Laah Swifatan min Swifwaatih, uk. 27
  • Imechapishwa: 01/07/2019